Loading...

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO.

Loading...
MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO.
link : MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO.

soma pia


MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii. 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Imemuachia huru Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Tido Mhando, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Hukumu hiyo imesomwa leo Januari 25.2019 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao dhidi ya mshtakiwa Tido. 

Katika kesi hiyo Tido ameshtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka wakati akiongoza shirika hilo ambapo anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na moja la kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. Milioni 800

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Shaidi amesema, upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake watano wameshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa kuwa kweli alitenda makosa hayo. 

Akiuchambua ushahidi huo, Hakimu Shaidi amesema miongoni mwa mambo mengi yaliyozungumzwa yalikuwa ni suala la mikataba.Amesema katika ushahidi wao, wa mkataba ulionyesha kulikuwa na sahihi ya Tido na Channel 2 lakini hakuna sahihi ya Mwanasheria Mkuu, Bodi wala mamlaka nyingine.

Ameongeza, Mshtakiwa Tido akiwa kama Mkurugenzi alikuwa ana wajibu wa kufata taratibu za zabuni na hivyo ili kitu kiwe mkataba lazima kipitie hatua lakini mkataba huo anaodaiwa kusaini Tido na Channel 2 hakuwa na sifa ya kuwa mikataba.

Akiendelea kuuchambua ushahidi huo Hakimu Shaidi amesema, ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hauelezi mahali ambapo malipo yamefanyikia, sababu malipo yamefanyika kwa mikataba ambayo haina vigezo.Upande wa mashitaka unadai mkataba huo haukufuata utaratibu wa kisheria.

" Kweli mkataba kuitwa mkataba ili ukamilike lazima kuwepo na watu ambao wanahusika na lazima kuwepo na mwanasheria hivyo mkataba huo sio halali bali ni makubaliano ya awali, " alisema.Baada ya uchambuzi huo, Hakimu Huruma alisema mshitakiwa huyo hakuna sehemu ilithibitisha kwamba ulikuwa ni mkataba hivyo anamwachia huru.

Miongoni mwa mashahidi wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi katika kesi hiyo ni ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

Katika kesi hiyo, inadaiwa Juni 16 mwaka Jana, huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume cha Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

Katika shtaka la pili, Tido anadaiwa kusaini makubaliano ya utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl.

Katika shtaka la tatu, anadaiwa Agosti 11 na Septemba mwaka Jana, akiwa Dubai, Tido alitumia vibaya madaraka yake kwa kusaini mkataba wa makubaliano ya ununuzi, usambazaji na kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.

Pia Tido anadaiwa, kutumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa makubaliano kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT Broadcast Infrastructure) kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI.

Katika shtaka la mwisho Tido anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16 mwaka huu akiwa UAE, aliisababishia TBC hasara ya Sh 887,122,219.19.


Hivyo makala MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO.

yaani makala yote MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/mahakama-yamuachia-huru-tido-mhando.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO."

Post a Comment

Loading...