Loading...

MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA

Loading...
MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA
link : MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA

soma pia


MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA

Magari yakionekana kupita katika daraja la Dumila ambalo liliathirika na mvua zilizonyesha usiku wa tarehe 15/1/2019, na kukata mawasiliano katika mkoa wa Morogoro na Dodoma kwa takriban saa 7.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati), mara baada ya kuwasili katika daraja la Dumila lililoathirika na mvua zilizonyesha usiku wa tarehe 15/1/2019 na kuvunja maingilio ya daraja hilo mkoani Morogoro.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dorothy Ntenga, akimueleza Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, hatua zilizochukuliwa na wakala huo katika matengenezo ya maingilio ya daraja la Dumila lililoathirika na mvua zilizonyesha usiku wa tarehe 15/1/2019, mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitazama athari za mvua zilizonyesha na kuharibu sehemu ya maingilio daraja la Dumila, mkoani Morogoro.
Kazi za ujazaji wa mawe na kokoto zilizokuwa zikifanyika katika kurekebisha athari za mvua zilizonyesha na kubomoa maingilio ya daraja la Dumila, mkoani Morogoro. Daraja hilo liko katika hatua za usanifu wa kina wa kuongeza tuta la daraja hilo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, amewahakikishia wananchi na watumiaji wa barabara ya Morogoro-Dodoma kuwa mawasiliano ya barabara hiyo sehemu ya maingilio ya daraja la Dumila yamerudi kama ilivyokuwa awali.

Kauli hiyo ameitoa leo mkoani Morogoro, alipofika darajani hapo kujionea athari za mvua zilizosababisha kubomoka kwa daraja hilo na wananchi kushindwa kutumia barabara hiyo kwa takriban masaa saba. 

"Kama mlivyoshuhudia tangu asubuhi tumeanza kazi za kurudisha mawasiliano katika barabara hii, matengenezo yakamilika na wananchi tayari wameshaanza kutumia barabara", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, ameupaongeza Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Morogoro, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kampuni ya ujenzi ya Yapi Merkez na wadau wote waliojitokeza katika kuhakikisha wanashirikiana bega kwa bega ili kurudisha mawasiliano katika eneo hilo.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanakuwa imara, Serikali ipo katika mpango wa kuboresha barabara hiyo ambapo kwa sasa wataalam wanafanya usanifu wa barabara hiyo na pindi usanifu huo utakapokamilika basi ujenzi wake utaanza mara moja na wataanza na sehemu korofi.

Awali akitoa taarifa kwa Naibu Waziri huyo, Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe, amesema kuwa uongozi wa mkoa ulifika eneo la tukio na kuanza kushirikiana na TANROADS mkoa kuhakikisha miundombinu hiyo inarejea mapema.Amewataka wananchi kujitolea kupanda matete na magugu maji katika eneo hilo ili kuelekeza maji yanayopita katika mto huo kuelekea sehemu husika.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dorothy Ntenga, amesema kuwa kazi zilizokuwa zikifanyika katika maingilio ya daraja hilo ilikuwa ni kuweka mawe makubwa na kokoto sehemu iliyobomoka.Amefafanua kuwa kutokana na sehemu hiyo kuwa na maji mengi na mchanga mwingi, wamefikiria kufanya usanifu wa daraja hilo utakaoleta suluhisho la kudumu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano



Hivyo makala MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA

yaani makala yote MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/mawasiliano-ya-barabara-ya-dodoma.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA"

Post a Comment

Loading...