Loading...
title : MH: JULIE MANNING: MWANAMKE MTANZANIA WA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUSOMEA SHERIA NCHINI MWENYE HISTORIA YA KIPEKEE NA REKODI LUKUKI!!!
link : MH: JULIE MANNING: MWANAMKE MTANZANIA WA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUSOMEA SHERIA NCHINI MWENYE HISTORIA YA KIPEKEE NA REKODI LUKUKI!!!
MH: JULIE MANNING: MWANAMKE MTANZANIA WA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUSOMEA SHERIA NCHINI MWENYE HISTORIA YA KIPEKEE NA REKODI LUKUKI!!!
1. Usuli:
Tanzania imebarikiwa kuwa na wanawake hodari na wachapakazi walioliletea heshima na mafanikio makubwa Taifa letu. Hata hivyo, weledi, utumishi uliotukuka, uzalendo pamoja na historia yake ya kipekee isiyo na mfanowe, ni vitu vinavyomtofautisha kabisa Bi. JULIE CATHERINE WILLIAM MANNING na wanawake wengine nchini!.
2. Asili ya BI.JULIE:
Bi.JULIE ni mmoja wa watoto 10 wa marehemu Dr. WILLIAM MANNING ambaye alikuwa chotara kwani baba yake alikuwa mzungu aliyemuoa Mwafrika Mmalawi(Bi. REBECCA MWALE). Bi. JULIE nae ni chotara kwani baba yake(Dr. WILLIAM), aliyezaliwa mwaka 1910, alimuoa mwanamke wa Msumbiji, Bi. MARIA REGINA ambaye ni mama yake Bi. JULIE.
Dr. WILLIAM na Bi. MARIA walifika Kyela, Mbeya zamani na kuishi kwenye nyumba ya serikali kwani Dr. WILLIAM alikuwa akihudumu kama daktari kwenye hospitali ya wilaya .
3. Masomo:
Dr. JULIE amesoma shule ya msingi Kissa ambayo ilikuwa katika eneo kati ya wilaya ya Kyela na Tukuyu. Shule hii ilikuwa ni ya masista.
Baada ya kumaliza elimu ya msingi, Bi. JULIE alifaulu vizuri hivyo akachaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya wasichana ya "Tabora Girls" huko Tabora, shule ambayo ilianzishwa mwaka 1928 ikiwa shule ya msingi na baadaye kubadilishwa na kuwa ya sekondari.
4. Chuo Kikuu:
Bi.JULIE alifaulu vizuri sana masomo yake na akawa na nia ya kuwa mwanasheria na wakati huo wa ukoloni hakukuwa na Chuo kikuu hapa nchini. Bahati nzuri, tarehe 25.10.1961, mwezi takribani mmoja kabla ya uhuru, kikazinduliwa Chuo Kikuu kipya jijini Dar Es Salaam . Chuo hicho kilikuwa na kitivo kimoja tu ambacho kilikuwa ni Kitivo cha Sheria. Chuo hicho kilikuwa ni "affiliate" ya Chuo Kikuu cha London na ndicho pekee kilichokuwa kinatoa kozi ya shahada ya sheria kwa nchi za Afrika Mashariki. Kitivo hicho kilizinduliwa na Mwalimu JK NYERERE, aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, ambaye alisema:
"My Government is so pleased that the law faculty is open before independence day. Dar Es Salaam is the only place where East Africans can get training in Law. It is not by accident that we started with a Law college. An essential part of national philosophy must be a Legal profession of great integrity which not only knows the formalities of Law but also understands the basic philosophy which underlies our society.."
Bi. JULIE alichaguliwa kujiunga na chuo hicho akiwa ni mmoja wa wanafunzi 13 wa kwanza wa Kitivo hicho cha Sheria walipotoka Tanganyika, Kenya na Uganda. Bi JULIE alikuwa ni mwanamke pekee kwenye Kitivo hicho. Hivyo, Bi. JULIE akawaameweka rekodi pacha ambapo alikuwa Mwanafunzi wa kwanza Mwanamke Tanganyika na pia Mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki kusomea shahada sheria.
Mkuu wa kwanza wa Kitivo hicho cha Sheria alikuwa ni Profesa Arther Brain Weston. Chuo hicho kilikuwa mtaa wa Lumumba ambapo jengo la Chuo hicho lilitolewa na TANU na Chuo kilikuwa na "Academic staff" 6 tu akiwemo Mganda 1. Kutokana na uhaba wa majengo, Mwalimu JK NYERERE alimfanyia mpango Bi. JULIE na hivyo akawaanaishi Ikulu. Mkenya SAMUEL KIVUITU, aliyekuja kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Kenya, ndiye alikuwa Kiongozi wa wanafunzi hao. Kuanzishwa kwa Kitivo hicho cha Sheria ndio ilikuwa chachu ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1970, eneo la Mlimani.
Bi. JULIE alimaliza shahada ya sheria mwaka 1963 na kuweka rekodi pacha nyingine ya kuwa Mwanamke Mtanzania wa kwanza kupata shahada ya sheria na pia Mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki kupata shahada hiyo chuoni hapo!.
Kwa hakika, ni rekodi ya kujivunia sana!.
5. Kuwa Mwandishi wa Sheria:
Baada ya kumaliza masomo yake, Bi. JULIE aliajiriwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kama Mwandishi wa Sheria, hivyo akaweka rekodi ya kuwa Mwanamke wa kwanza Mtanzania msomi kufanya kazi hiyo.
6. Kufiwa na Baba yake:
Tarehe 28.4.1971, Bi.JULIE alifiwa na baba yake, Dr. WILLIAM MANNING, aliyekuwa akijivunia sana mafanikio hayo makubwa ya mwanae. Dr. WILLIAM, aliyefariki kutokana na ugonjwa wa asthma, alizikwa hukohuko Mbeya. Bi. JULIE aliendelea kuchapa kazi kwa bidii ikiwa ni njia mojawapo ya kumuenzi marehemu baba yake aliyeamini kuwa kazi ni msingi wa maendeleo.
7. Kuteuliwa Ujaji:
Mwaka 1973, Bi. JULIE MANNING aliweka rekodi nyingine pacha pale alipoteuliwa na Rais JK NYERERE kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Tanzania. Bi. JULIE akawa Mwanamke wa kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kuwa Jaji!. Uteuzi huu ulitikisa Afrika Mashariki nzima ambapo gazeti la tarehe 7.5.1973 liliipa habari hiyo kipaumbele kwenye ukurasa wa kwanza: "WOMAN MADE JUDGE!!!!".
8. Kuteuliwa Uwaziri:
Mwishoni mwa Octoba, 1975, Bi. JULIE aliitwa Ikulu na Rais JK NYERERE ambaye alimjulisha kwamba amemteua kuwa Mbunge wa Taifa, kwa kutumia moja kati ya nafasi 10 alizonazo Rais chini ya Katiba.
Aidha, Jumapili ya tarehe 9.11.1975, Rais NYERERE alimteua Bi. JULIE kuwa Waziri wa Sheria. Bi. JULIE na Bi. TABITHA IJUMBA MWAMBENJA SIWALE, ambaye katika Baraza hilo jipya la Mawaziri aliteuliwa kuwa Waziri pia, ndio wanawake wa kwanza kuwa Mawaziri kamili nchini. Hii ni kwasababu katikati ya miaka ya 1960s, Bi. TITI MOHAMED aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni na Bi. LUCY LAMECK kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Afya. Kabla ya uteuzi huo wa Bi. JULIE, hakukuwa na Waziri wa Sheria. Kwa hakika ilikuwa ni heshima kubwa sana kuamini wa na Baba wa Taifa na kupewa wadhifa mkubwa kama huo.
Tarehe 21.12.1975, Bi. JULIE 'alilimwa' barua na Mh. ABRAHMAN BABU. Mh. BABU alikuwa amewekwa kizuizini gereza la Ukonga ambapo yeye na wenzake pamoja na waliokuwa wakishikiliwa Zanzibar, walidaiwa kuwa walihusika na mauaji ya marehemu Rais ABEID AMAN KARUME yaliyotokea tarehe 7.4.1972.
Mh. BABU aliandika barua hiyo baada ya tahariri ya gazeti la Daily News la tarehe 18.11.1975 kueleza: "Maharamia wateswe ili wakiri makosa yao! .
Ndipo BABU akaandika:
" Mwandishi wa tahariri haelewi kuwa ikiwa leo tutakubali maharamia wateswe, kesho itakuwa zamu ya wahariri kuteswa. Rais NYERERE anakasirishwa sana na utesaji na umwagaji damu. Sasa akifa akaja kurithiwa na mtu mwenye maadili ya Pakashume, ikiwa Mrithi huyo atarithi taasisi zilizopotoka kimaadili basi maadili yote ya kisiasa na kijamii yatakuwa ya kipakashume, ikiwa atarithi taasisi zilizopotoka kimaadili. Kwavile sasa Wizara ya Sheria imepata Waziri, tuna imani haki itatendeka..".
Hizi zilikuwa changamoto za mwanzo alizokumbana nazo Mh. Waziri JULIE MANNING ambazo zilimsaidia kumkomaza haraka.
Bi. JULIE alikuwa Waziri wa Sheria hadi 1983.
9. Kuteuliwa Kamishna wa Tume ya Uchaguzi
Bi.JULIE aliweka rekodi nyingine pale alipoteuliwa kuwa miongoni mwa Makamishina 7 wa kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambapo alikuwa Mwanamke pekee. Makamishina wengine walikuwa ni Mh. LEWIS MAKAME, MARK BOMANI, AUGUSTINO RAMADHANI, SOLOMON LIANI, BEN LOBULU na MASAUNI YUSUPH MASAUNI.
Tume hii iliundwa na Mh. Rais kwa mujibu wa Kifungu cha 74 cha Katiba ya Tanzania, 1977.
10. Kuteuliwa Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini:
Bi. JULIE aliteuliwa kuwa mmoja wa makamishina wa Tume ya Kurekebisha sheria nchini, kazi ambayo amelifanya kwa miaka mingi.
11. Mjumbe wa Taasisi ya Dini
Bi. JULIE, si tu kwamba amebobea kwenye mambo ya siasa tu bali pia mambo ya dini na ni Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya "Young Women Christian Association of Tanzania".
12. Kupewa Medali na Rais JM KIKWETE:
Ijumaa ya tarehe 9.12.2011, kulifanyika hafla kubwa ya kukata na shoka ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru. Moja ya matukio makubwa siku hiyo ilikuwa ni utunuku wa Tuzo na Medali kwa Watanzania waliotoa mchango mkubwa katika Taifa hili kwa utumishi wao uliotukuka. Bi. JULIE alikuwa mmoja wa waliotunukiwa medali ya aina yake siku hiyo na Rais wa awamu ya nne, Mh. Dr. JAKAYA MRISHO KIKWETE!.
13. Kupewa Tuzo na Rais KIKWETE ya kuwa Mwanamke wa kwanza kusomea sheria:
Tarehe 25.10.2011, Kitivo cha Sheria, Udsm, kiliandaa kumbukizi ya miaka 50 ya kuanzisha kwa Kitivo hicho: "Golden Jubilee Celebrations of the Faculty of Law:-25th October 1961-25th October 2011.
Kumbukizi hilo lilikuwa la aina yake ambapo wanafunzi wote waliosoma Kitivo hicho toka kinaanzishwa walialikwa. Aidha, zilitolewa tuzo mbalimbali. Majina ya Wanafunzi wote Bora wa Kitivo hicho toka kinasnzishwa tarehe 25.10.1961 (First Class Honours Degree Holders) ambao walipata GPA ya 4.4-5.0 yalitangazwa, miongoni mwao ni:
1. Mutula Kilonzo (Kenya)
2. Hassan Boubacar Jallow (Gambia)
3. Dr. Ringo Tenga (TZ)
4. Dr. Masumbuko Lamwai (TZ)
5. Dr. Asha Rose Migiro (TZ)
6. Eric Ng'imaryo (TZ)
7. Prof. Palamagamba Kabudi (TZ)
8. Prof. Hamudi Majamba (TZ)
9. Steven Mosha (TZ & Uganda).
Aidha, Prof. PALAMAGAMBA AIDAN MWALUKO KABUDI alipewa Tuzo maalum ya kipekee kwani GPA yake ya 4.9 ndiyo bora kuliko zote toka Kitivo hicho kianzishwe. Pia, ilibainika kuwa licha ya Kitivo hicho kuwa kikongwe kuliko vyote chuoni hapo, lakini ni wanafunzi wachache mno waliopata "First Class" na wanafunzi wa mwisho waliipata mwaka 1992!. Hii ni tofauti na vitivo vingine ambako "First Class" ni za kumwaga!.
Siku hiyo ya kipekee ya utoaji zawadi, Bi. JULIE alitunukiwa na Dr. GHALIB BILAL Tuzo ya kuwa Mwanamke wa Kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kupata shahada ya sheria katika Kitivo cha Sheria hapa nchini!
Huyu ndiye Bi. JULIE CATHERINE WILLIAM MANNING, Mwanamke mwenye rekodi nyingi na historia ya kipekee aliyetunukiwa medali kutokana na utumishi uliotukuka kwa nchi yake.
Hivyo makala MH: JULIE MANNING: MWANAMKE MTANZANIA WA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUSOMEA SHERIA NCHINI MWENYE HISTORIA YA KIPEKEE NA REKODI LUKUKI!!!
yaani makala yote MH: JULIE MANNING: MWANAMKE MTANZANIA WA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUSOMEA SHERIA NCHINI MWENYE HISTORIA YA KIPEKEE NA REKODI LUKUKI!!! Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MH: JULIE MANNING: MWANAMKE MTANZANIA WA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUSOMEA SHERIA NCHINI MWENYE HISTORIA YA KIPEKEE NA REKODI LUKUKI!!! mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/mh-julie-manning-mwanamke-mtanzania-wa.html
0 Response to "MH: JULIE MANNING: MWANAMKE MTANZANIA WA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUSOMEA SHERIA NCHINI MWENYE HISTORIA YA KIPEKEE NA REKODI LUKUKI!!!"
Post a Comment