Loading...
title : MTOTO WA TEMBO ALIYETUMBUKIA SHIMONI AOKOLEWA PORI LA AKIBA LWAFI
link : MTOTO WA TEMBO ALIYETUMBUKIA SHIMONI AOKOLEWA PORI LA AKIBA LWAFI
MTOTO WA TEMBO ALIYETUMBUKIA SHIMONI AOKOLEWA PORI LA AKIBA LWAFI
Mamlaka ya Usimamizi wanyamapori Tanzania, inapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa mnamo tarehe 11/01/2019 majira ya saa kumi kamili jioni (10:00) Ungozi wa Pori la Akiba Lwafi Mkoani Katavi walipokea taarifa kutoka kwa Bw.Salum Summy ambaye ni mmiliki wa shamba la Msipazi linalopakana na pori hilo kuhusu kunasa kwa mtoto wa tembo kwenye tope aliyetumbukia ndani ya chimo eneo la china ndani ya pori hilo.
Bw. Salum alipata taarifa hizo kutoka kwa wafanyakazi wake waliyokuwa jirani baada ya kusikia tembo wakipiga kelele kwa sauti zaidi ya saa moja, na baada ya kufuatilia wakaona kundi kubwa la tembo wakijitahidi kumtoa mtoto wao kwenye shimo. Kwa vile tembo walikuwa wengi watu hao hawakuweza kuwasogelea, hivyo waliamua kuwasiliana na uongozi wa Pori la Lwafi kuhusu tukio hilo . Waliwasiliana na Mkuu wa Kanda ya Lwafi Bw. Asubuhi T. Kasunga,na kumueleza taarifa hiyo, Bw. Asubuhi bila kuchelewa aliondoka akiongozana na askari 4 wakiwa na siraha na mahema kuelekea eneo la tukio, walifika majira ya saa 5:00 usiku na kupata taarifa ya awali toka kwa mashuhuda wa tukio hilo,
Kwa vile ilikuwa usiku sana na kuhofia kuwepo kwa tembo wengine jirani walisubiri hadi kupambazuke hadi tarehe 12/1/2019 majira ya saa 12:00 asubuhi walifuatana na wafanyakazi wa shamba pamoja na wanakijiji jumla walikuwa 11 walifika eneo la tukio na kumkuta mtoto wa tembo mwenye umri chini ya wa mwaka mmoja akiangaika kutoka shimoni. Jitihada za kumuokoa zilifanyika baada ya kupanga mawe ndani ya shimo bila kumdhuru mtoto,na hatimaye walimtoa mtoto.
Baada ya kumtoa walimpelea hadi kambi ya Shamba la Msipazi. Waliwahoji wafanyakazi kujua tembo wanaonekana muda gani kusudi waweze kumrudisha mtoto kwenye kundi, walidai kawaida wanapita majira ya saa nne usiku walisubiri siku nzima hadi muda huo lakini hawakuonekana. Tembo hao.
Muda wote walikuwa wakiwasiliana na Dakitari wa tiba za wanyamapori toka Shirika la Uhifadhi liitwalo (Wildlife Conservation Society-WCS) Bi. Elizabert Stigmaier kutoa ushauri wa chakula cha kumlisha mtoto huyo maana alionekana amechoka. Wakaelezwa wampatie Glucose aina ya DNS na aliwaeleza jinsi ya kumpa ilia pate nguvu.
Tarehe 13/1/2019 Ofisi yangu iliwasiliana na wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa wanyamapori (TAWIRI ). Idara ya wanyamapori,na WCS na kufikia uamuzi wa tumsafirishe kwa ndege ya kampuni ya Northen Air Transport No. 5G-DEB ambayo ilitolewa na Rusell Hastings wa Shirika la Uhifadhi liitwalo ‘ Freidkin Conservation’ hadi Arusha majira ya saa 10: 00 jioni na kupelekwa kwenye kituo cha kupokea Wanyamapori yatima kiitwacho ‘ Makoa farm Vertinary Clinic’ iliyopo Machame Wilaya ya Hai.Mtoto huyo wa tembo anaendelea vizuri.
LIMETOLEWA NA
Dkt. JAMES WAKIBARA (KAMISHNA MHIFADHI-TAWA)
Hivyo makala MTOTO WA TEMBO ALIYETUMBUKIA SHIMONI AOKOLEWA PORI LA AKIBA LWAFI
yaani makala yote MTOTO WA TEMBO ALIYETUMBUKIA SHIMONI AOKOLEWA PORI LA AKIBA LWAFI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MTOTO WA TEMBO ALIYETUMBUKIA SHIMONI AOKOLEWA PORI LA AKIBA LWAFI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/mtoto-wa-tembo-aliyetumbukia-shimoni.html
0 Response to "MTOTO WA TEMBO ALIYETUMBUKIA SHIMONI AOKOLEWA PORI LA AKIBA LWAFI"
Post a Comment