Loading...
title : POLISI KILIMANJARO YANASA DAWA ZA KULEVYA KILO 80.
link : POLISI KILIMANJARO YANASA DAWA ZA KULEVYA KILO 80.
POLISI KILIMANJARO YANASA DAWA ZA KULEVYA KILO 80.
Anaandika Dixon Busagaga,Moshi.
KIKOSI cha Pikipiki cha jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kimefanikiwa kukamata kilogramu 80 za Dawa za Kulevya aina ya Mirungi iliyokuwa ikisafirishwa kwa kutumia pikipiki kutoka nchi jirani ya Kenya kuelekea mkoa wa Arusha.
Majani hayo ya Miringi yaliyokuwa yamefungwa katika vifurushi vidogo vidogo zaidi ya 50 na kisha kuwekwa kwenye mfuko mmmoja mkubwa maarufu kama Kiroba yalipatikana baada ya askari Polisi kujaribu kumkimbiza msafirishaji wa Mirungi ambaye alitekeleza pikipiki na mzigo huo.
Kamanda wa Polisi mkao wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issa alithibitisha kukamatwa kwa Dawa hizo za kulevya katika eneo la Uchira ambapo msafirishaji huyo alifanikiwa kukimbia na kuiacha pikipiki aliyokuwa akitumia.
“Mkoa wa Kilimanjaro kumekuwa na tatizo kubwa sana, linalohusiana na usafirishaji wa Mirungi na wasafirishaji wamekuwa wakitumia barabara kuu, sasa askari wa pikipiki ambao wanafanya kazi hii ya kufukuzana na hawa watu wa mirungi wamefanikiwa kukamata kilogramu 80 za Mirungi”alisema Issah.
Alisema kundi la wasafirishaji wa Dawa hizo za kulevya ambao wamekuwa wakisafirisha kutoka nchi ya Kenya kupitia mpaka wa Holili pindi linapoingia barabarani limeonekana kuwa tishio na hatari kwa usalama wa watu wengine barabarani kwa namna wanavyoendesha pikipiki zao.
“Siku ya leo(Jana) imekamatwa pikipiki moja yenye namba MC 168 CAZ ambayo imetoka nchini Kenya lakini ni ya Tanzania na ikiwa na gunia moja kubwa lenye uzito wa kilo 80,nah ii inaonyesha ilikuwa bado hawajagawana kabisa lakini askari wetu kwa ushujaa wao wamewafukuza hawa watu na matokeo yake wamekamata”alisema Issah .
Kamanda Issah alisema baada ya kufungua mfuko huo walibaini uwepo wa vifurushi vingi vikiwa vimefungwa Majani ya Mirungi kwa njia tofauti tofauti huku ikiwa imepewa majina maalumu ya wahusika wa Dawa hizo.
MIrungi hiyo naona ilivyohifadhiwa na watuhumiwa hao tayari kwa kusafirishwa.
Kamanda wa Polisi mkao wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issa akionesha Dawa za kulevya aina ya Mirungi walioikamata eneo la Uchira,ambapo msafirishaji huyo alifanikiwa kukimbia na kuiacha pikipiki aliyokuwa akitumia.
Mirungi iliyokamatwa ikikusanywa na kuwekwa vizuri
Hivyo makala POLISI KILIMANJARO YANASA DAWA ZA KULEVYA KILO 80.
yaani makala yote POLISI KILIMANJARO YANASA DAWA ZA KULEVYA KILO 80. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala POLISI KILIMANJARO YANASA DAWA ZA KULEVYA KILO 80. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/polisi-kilimanjaro-yanasa-dawa-za.html
0 Response to "POLISI KILIMANJARO YANASA DAWA ZA KULEVYA KILO 80."
Post a Comment