Loading...

Serikali Yashinda Kesi Dhidi ya Wanaharakati Kuhusu Kanuni za Maudhui Mitandaoni

Loading...
Serikali Yashinda Kesi Dhidi ya Wanaharakati Kuhusu Kanuni za Maudhui Mitandaoni - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Serikali Yashinda Kesi Dhidi ya Wanaharakati Kuhusu Kanuni za Maudhui Mitandaoni, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Serikali Yashinda Kesi Dhidi ya Wanaharakati Kuhusu Kanuni za Maudhui Mitandaoni
link : Serikali Yashinda Kesi Dhidi ya Wanaharakati Kuhusu Kanuni za Maudhui Mitandaoni

soma pia


Serikali Yashinda Kesi Dhidi ya Wanaharakati Kuhusu Kanuni za Maudhui Mitandaoni


Na: Beatrice Lyimo, MAELEZO

Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imehukumu kwamba Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo hakukosea wala kukiuka Katiba kwa kutunga Kanuni za Maudhui Mitandaoni za mwaka 2018.

Hayo yamejidhihirisha baada ya Mahakama hiyo kusikiliza na hatimaye kuitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu, Bodi ya Wadhamini wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mtandao wa Watetea Haki za Binadamu Tanzania (Human Rights Defenders Coalition) dhidi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Katika shauri hilo walalamikaji wameshindwa kuthibitisha jinsi gani Kanuni hizo zitakavyo athiri haki za msingi za Walalamikaji katika masuala ya uhuru wa habari na mawasiliano ya mitandaoni.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa leo Januari 9, 2019 Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, imekubaliana na hoja za Mawakili wa Serikali kuwa Kanuni za Maudhui Mtandaoni zimetungwa kwa mujibu wa sheria na kupelekea Mahakama hiyo kutupilia mbali shauri hilo.

Shauri hilo liliendeshwa na mawakili kutoka Ofisi Mpya ya Wakili Mkuu wa Serikali ambao ni Bibi Alesia Mbuya, Bw. Ladislaus Komanya, Bw. Sylvester Mwakitalu, Bw. Johanes Kalungura, Bw. Killey Mwitasi, Bw. Abubakar Mrisha na Bibi Neisha Shao ambapo upande wa walalamikaji waliwakilishwa na mawakili Fulgence Masawe, James Marenga na Jeremia Mtobyesa.

Kwa hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Septemba 4, 2018, sasa ni rasmi madai ya kwamba Kanuni hizo zinabana uhuru wa habari na kwamba zilitungwa kimakosa yaaanguka rasmi.


Hivyo makala Serikali Yashinda Kesi Dhidi ya Wanaharakati Kuhusu Kanuni za Maudhui Mitandaoni

yaani makala yote Serikali Yashinda Kesi Dhidi ya Wanaharakati Kuhusu Kanuni za Maudhui Mitandaoni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Yashinda Kesi Dhidi ya Wanaharakati Kuhusu Kanuni za Maudhui Mitandaoni mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/serikali-yashinda-kesi-dhidi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Serikali Yashinda Kesi Dhidi ya Wanaharakati Kuhusu Kanuni za Maudhui Mitandaoni"

Post a Comment

Loading...