Loading...
title : Tanzania ina chakula cha ziada na imejitosheleza- Waziri wa Kilimo Hasunga
link : Tanzania ina chakula cha ziada na imejitosheleza- Waziri wa Kilimo Hasunga
Tanzania ina chakula cha ziada na imejitosheleza- Waziri wa Kilimo Hasunga
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Kwa mliganisho wa mahitaji na uzalishaji nchi ina ziada ya tani 3,013,515 na imejitosheleza kwa asilimia 123 na 120 mtawalia ambapo uzalishaji katika msimu wa 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa tani 15,900,864 na 16,172,841 mtawalia ambapo mahitaji ya chakula yanayoendana na uzalishaji huo ni tani 13,159,326, na 13,300,034 kwa mwaka wa ulaji 2017/2018 na 2016/2017 mtawalia.
Uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa uzalishaji wa 2017/2018 ulifikia tani 16,981,974 zikiwemo tani tani 9,537,857 za mazao ya nafaka na tani 7,354,117 mazao yasiyo nafaka, kiwango ambacho kimeiwezesha nchi kutosheleza mahitaji yake ya chakula ya tani 13,569,285 katika mwaka 2018/2019 kwa kiwango cha utoshelevu (Self Sufficiency Ratio-SSR) cha asilimia 124.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 2 Januari 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma.
Alisema Uzalishaji wa mahindi katika msimu wa 2017/2018, 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa ni tani 6,273,150; 6,680,758 na 6,148,699 mtawalia, wakati mahitaji yanayoendana na uzalishaji huo ni tani 5,462,390; 5,407,499 na 5,202,405 katika miaka ya ulaji ya 2018/2019, 2017/2018 na 2016/2017, Ambapo ziada ya tani 810,760(2018/2019); 1,273,259(2017/2018) na 946,284(2016/2017) zilipatikana.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma tarehe 2 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).
Hivyo makala Tanzania ina chakula cha ziada na imejitosheleza- Waziri wa Kilimo Hasunga
yaani makala yote Tanzania ina chakula cha ziada na imejitosheleza- Waziri wa Kilimo Hasunga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tanzania ina chakula cha ziada na imejitosheleza- Waziri wa Kilimo Hasunga mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/tanzania-ina-chakula-cha-ziada-na.html
0 Response to "Tanzania ina chakula cha ziada na imejitosheleza- Waziri wa Kilimo Hasunga"
Post a Comment