Loading...

TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE.

Loading...
TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE.
link : TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE.

soma pia


TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE.

Mkutano wa waandishi wote wa habari za michezo unatarajiwa kufanyika Jumapili Februari 10 mwaka huu kujadili Rasimu ya Kwanza ya Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA).

Kabla ya mkutano huo wa wadau wa habari za michezo, pia kutafanyika mkutano wa wahariri wa habari za michezo Februari 6 mwaka huu, lengo ikiwa ni kupitia rasimu hiyo kwa pamoja kabla ya kuifikisha kwa wadau wengine. Mikutano yote itafanyika Dar es Salaam, lakini ukumbi utatangazwa hivi karibuni.

Ni imani ya Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya TASWA kwamba mikutano hiyo yote miwili itakuwa na tija na itakuwa muongozo mzuri katika kuandaa Katiba bora kwa maslahi mapana ya waandishi wa habari za michezo nchini. Hivyo kamati inawaomba waandishi wote wa habari za michezo wajitokeze kwa wingi , ili kwa pamoja wajadili namna ya kuboresha rasimu ambayo ilitolewa Desemba 9 mwaka jana.

Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya TASWA imeandaa mapendekezo ya rasimu iliyoandaliwa kwa kuangalia Katiba za vyama mbalimbali duniani vinavyohusiana na waandishi wa habari za michezo na pia kupitia muongozo kutoka Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS), ambacho TASWA ni mwanachama.

Pia Kamati imechambua Katiba ya sasa ya TASWA na kupokea maoni kutoka kwa waandishi wa habari za michezo kuhusu maeneo yenye upungufu kwa nia ya kuiboresha.

Maeneo mbalimbali yamefanyiwa kazi katika rasimu hiyo baadhi yakiwa ni sifa za mwanachama, wajibu wa mwanachama, muundo wa uongozi, sifa za viongozi na pia ukomo wa uongozi. Pia kuna mapendekezo katika rasimu hiyo ya kuanzishwa kamati mbalimbali kwa nia ya kuisaidia Kamati ya Utendaji.

Kamati ya Katiba ya TASWA imeundwa kutokana na agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe aliyeitaka BMT isitishe uchaguzi wa TASWA uliokuwa umepangwa kufanyika Novemba 25 mwaka jana na badala yake BMT ikutane na viongozi wa TASWA pamoja na baadhi ya wanahabari wa michezo kuona namna ya kuifanyia marekebisho Katiba ya TASWA iendane na wakati.

Nawasilisha,Amir Mhando
Katibu wa Kamati ya Katiba/ Katibu Mkuu TASWA


Hivyo makala TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE.

yaani makala yote TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/taswa-yaitisha-mkutano-kwa-wanachama.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE."

Post a Comment

Loading...