Loading...

WILAYA YA CHEMBA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO

Loading...
WILAYA YA CHEMBA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WILAYA YA CHEMBA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WILAYA YA CHEMBA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO
link : WILAYA YA CHEMBA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO

soma pia


WILAYA YA CHEMBA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO

Na Shani Amanzi, Chemba

Mkuu wa wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amewaonya watu watakaotaka kufanya udanganyifu katika zoezi la ugawaji vitambulisho kwa Wajasiliamali Wadogo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwani watakuwa wamekwenda kinyume na taratibu. 

Dc Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa anazindua zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho kwa Wajasirimali Wadogo wilayani Chemba hivi karibuni katika Ukumbi wa Godown. 

“Nataka zoezi hili lisizidi siku saba na kuhakikisha mapato yanaenda vizuri bila kusahau kuhakikisha makundi ya Wajasirimali Wadogo wanapata ikiwemo wa Magenge ya chakula,Mitumba,Mafundi cherehani,Wasusi na wengineo wanaostahili katika Tarafa zote ikiwemo Mondo,Goima,Kwamtoro na Farkwa za Chemba”alisema Dc Odunga. 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba alisema kuwa katika zoezi la awali walitambua Wajasiliamali 105 ambapo katika kata ya Chemba walipata Wajasirimali 35,kata ya Kidoka Wajasirimali 40,kata ya Paranga Wajasiliamali 30 na kuwa zoezi hilo limehakikiwa na Kitengo cha Biashara kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi pamoja na Maendeleo ya Jamii. 

Aidha Dkt.Semistatus H.Mashimba amesema” Kamati ya zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho kwa Wajasiliamali Wadogo ilizungunga wilaya nzima katika kutoa elimu na kuhakikisha zoezi hili linakuwa endelevu na tulibaini kuna watu walitaka kufanya udanganyifu na tuliweza kutatua jambo hilo na kuhakikisha hali hiyo haitatokea tena” 

Jumla ya Vitambulisho vya Wajasirimali Wadogo 2750 kutoka Ofisi ya Rais –Tamisemi viligaiwa Mkoani ambapo walikabidhi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mhe.Odunga ambapo aliagiza Mkurugenzi Dkt.Mashimba kuratibu zoezi hilo la Ugawaji Vitambulisho kwa wilaya yake. 
 Mkuu wa wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akizungumza wakati anazindua zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho kwa Wajasirimali Wadogo wilayani Chemba hivi karibuni katika Ukumbi wa Godow,Dc Odunga amewaonya watu watakaotaka kufanya udanganyifu katika zoezi hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
 Mkuu wa wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akigawa Vitambulisho kwa baadhi ya Wajasiliamali Wadogo,wakati wa uzinduzi wilayani Chemba hivi karibuni katika Ukumbi wa Godow,pichani kulia anaeshuhudia ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo Mh.Zahara Muhidin Michuzi
Baadhi ya Wajasiliamali Wadogo wadogo wakiwa wamejitokeza kwenye uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho hivyo. 


Hivyo makala WILAYA YA CHEMBA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO

yaani makala yote WILAYA YA CHEMBA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WILAYA YA CHEMBA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/wilaya-ya-chemba-yazindua-zoezi-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WILAYA YA CHEMBA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO"

Post a Comment

Loading...