Loading...
title : MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AVUNJA KAMATI YA UJENZI
link : MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AVUNJA KAMATI YA UJENZI
MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AVUNJA KAMATI YA UJENZI
Na Shani Amanzi, Chemba.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga achukizwa na Wananchi na Wafanyakazi wa Serikali wasiokuwa wawijibikaji hasa pale wanapopewa majukumu na Serikali ikiwemo kuwekwa kwenye Kamati za shughuli za kimaendeleo katika jamii.
Odunga aliyazungumza hayo alipotembelea kata ya mrijo akiongozana na mkurugenzi wa Halmashauri, Katibu Tawala pamoja na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo,Tarehe 12/1/2019.
Amesema “nampongeza Rais wa Awamu ya Tano Mhe.John Pombe Magufuli kwa kuweka kipaumbele katika Afya na kutaka kila kata kuwe na Kituo cha Afya na sitakubali mwananchi au mtaalam yoyote akwamishe malengo hayo kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa”
Aidha Mhe.Odunga aliongeza kwa kusema mkumbuke wapo Wananchi ambao baadhi yao wapo macho na wanataka kushirikishwa katika kila jambo na inasikitisha sana Kamati hii ya Ujenzi inafanya mambo bila kuwashirikisha Wananchi na ninaamuru Kamati hii ivunjwe na kutaka Mkurugenzi ahakikishe anaunda nyingine mara moja kuanzia leo kwani wengi wao wananchi hawaiamini Kamati hii ikiwemo na upande wa manunuzi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba Dkt.Semistatus.H.Mashimba ameomba ushirikiano kwa Wananchi katika kuhakikisha Ujenzi wa Kituo cha Afya- Mrijo kinakamilika na kuipongeza Serikali katika kuweka kipaumbele Chemba katika Ujenzi wa Vituo vya Afya.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga wa pilia kushoto akizungumza na wananchi (hawapo pichani) no baada ya kuitembelea kata ya mrijo akiongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri (wa pili kulia) Mh.Dkt.Semistatus Mashimba pamoja na Katibu Tawala Zahara Muhidin Michuzi (mwisho kushoto) sambamba na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo,Tarehe 12/1/2019.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akizungumza na baadhi ya Wananchi alipotembelea kata ya mrijo akiongozana na mkurugenzi wa Halmashauri, Katibu Tawala pamoja na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo,Tarehe 12/1/2019.
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Mrijo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nano baada ya kuitembelea kata ya mrijo akiongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri, Mh.Dkt.Semistatus Mashimba pamoja na Katibu Tawala Zahara Muhidin Michuzi sambamba na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo,Tarehe 12/1/2019.
Hivyo makala MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AVUNJA KAMATI YA UJENZI
yaani makala yote MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AVUNJA KAMATI YA UJENZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AVUNJA KAMATI YA UJENZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/mkuu-wa-wilaya-ya-chemba-avunja-kamati.html
0 Response to "MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AVUNJA KAMATI YA UJENZI"
Post a Comment