Loading...
title : BULAYA AENDELEA NA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI INAYOTEKELEZWA KUPITIA MFUKO WA JIMBO
link : BULAYA AENDELEA NA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI INAYOTEKELEZWA KUPITIA MFUKO WA JIMBO
BULAYA AENDELEA NA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI INAYOTEKELEZWA KUPITIA MFUKO WA JIMBO
Mh. Ester Bulaya ameendelea na ziara yake jimboni na siku ya Jana ameshiriki kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo inayofadhiriwa mfuko wa jimbo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na kuzungumza na wananchi pamoja na Wanafunzi.
Mapema majira ya 5:00 asubuhi Mh. Mbunge alifika katika shule ya Msingi Kilimani kwaajili ya ukaguzi wa mradi wa Ujenzi wa Choo chenye jumla ya matundu 12 yaani me 6 na ke 6 ambapo mh. Mbunge kupitia fedha ya mfuko wa jimbo alichangia tsh milioni nne (4,000,000/=) ili kuwapunguzia wazazi michango ambayo ilionekana kuwa kero kwa wananchi wa maeneo ya Nyasura.
Aidha mh. Mbunge baada ya kusomewa taarifa ya ujenzi wa choo husika kupitia mwl. mkuu wa shule akawiwa na usimamizi mzuri wa fedha husika na kuamua kutoa tsh 800,000/= fedha toka mfukoni kwaajili ya umaliziaji wa choo husika kwa kupaka langi na uwekaji wa milango ili choo hicho kianze kutumika kwa uharaka kwani nikweli kuwa wanafunzi wamekuwa wakipata adha kwa muda mrefu.
Mh. Mbunge alitoa nafasi kwa wanafunzi kwaajili ya kutoa changamoto zinazowakabili ndipo alisimama mwanafunzi mmoja kwa niaba ya wanafunzi wenziwe na kutoa changamoto ya kutokuwa na mpira wa miguu ambapo mh. Mbunge akatoa tsh 50,000/= kwaajili ya ununuzi wa mpira na kuhaidi kuleta jezi kwa upande wa football na Netball ili wanafunzi wazitumie wakati wa michezo.
Nae mwl. mkuu wa shule ya msingi Kilimani akishukru kwa niaba ya kamati ya shule alisema anashukru sana kwa ujio wa mh. Mbunge kukagua fedha zake zinatumikaje lakini pia anashukru kwa kukumbukwa tena kwa kupewa fedha awamu ya pili katika shule hiyo kwani mwaka wa fedha 2016/17 shule hiyo pia ilipewa fedha kwaajili ya uezekaji Darasa na 2017/18 ujenzi wa choo hivyo mh. Mbunge aendelee kuwaunga mkono tena na tena.
Mh. Mbunge akiambatana na mh. Diwani wa kata ya Nyasura aliendelea na ziara ya kukagua ujenzi wa darasa katika Shule ya msingi Nyasura ambapo kupitia fedha ya Mfuko wa jimbo kwa mwaka wa fedha 2017/18 aliombwa kuchangia tsh 910,000/= kwaajili ya kumalizia upauaji wa Darasa husika na sasa Darasa limemalizika kwa hatua ya upauaji na linatumika kutokana na upungufu wa Madarasa uliopa shuleni hapo.
Baadae jioni mh. Mbunge alielekea katika Kata ya Nyatwali ambapo alizungumza wananchi na kupokea kero za wananchi na hatimae kutoa mrejesho kwa wananchi juu ya shughuli mbali mbali za maendeleo katika Kata ya Nyatwali.
Aidha wakati mh. Mbunge akipokea kero za wananchi ilizuka kero ya wananchi kuhamishwa ndipo mh. Mbunge akaamua kuwauliza kwa kauli moja kuwa anaomba ajue wanaotaka kulipwa na kuhamishwa wanyooshe mikono na wanaotaka kubaki pia, wananchi wote kwa pamoja walikubaliana kuwa hawako tayari kuhamishwa na kumuomba mh. Mbunge awasaidie kuwawakilisha ili wasihamishwe katika makazi yao waliyoyazoea.
Mh. Mbunge Leo ataendelea na ziara katika kijiji cha Bukore, Tairo, Sazira na baadae kijiji cha bitaraguru kwa kuzungumza na wananchi na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo inayofadhiriwa na fedha ya mfuko wa jimbo
Hivyo makala BULAYA AENDELEA NA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI INAYOTEKELEZWA KUPITIA MFUKO WA JIMBO
yaani makala yote BULAYA AENDELEA NA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI INAYOTEKELEZWA KUPITIA MFUKO WA JIMBO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BULAYA AENDELEA NA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI INAYOTEKELEZWA KUPITIA MFUKO WA JIMBO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/bulaya-aendelea-na-ziara-ya-kukagua.html
0 Response to "BULAYA AENDELEA NA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI INAYOTEKELEZWA KUPITIA MFUKO WA JIMBO"
Post a Comment