Loading...

CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA

Loading...
CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA
link : CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA

soma pia


CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA


NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE 

KATIKA kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 42 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kata ya Pera Chalinze, Bagamoyo, Shawali Ndembo amekihama chama hicho na kukimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Pia wanachama wengine wanne kutoka chama hicho wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM. 

Akimpokea Ndembo wakati wa sherehe za maadhimisho hayo wilaya ya Bagamoyo, yaliyofanyika Pingo kata ya Pera, mwenyekiti wa CCM Bagamoyo, Abdulsharif Zahoro alisema ilani ya chama inatekelezwa na kuleta heshima kwa wananchi. 

Alisema, serikali ya awamu ya tano inaitendea haki ilani hiyo hivyo kazi kubwa kwa wanaCCM ni kuisemea serikali kwa yale inayotekeleza na kutatua changamoto mbalimbali kwa watanzania. "Nampongeza mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, Dk.John Magufuli kwa kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo "alisema Sharif. 

Sharif ,alisema uongozi ni dhamana mwenyekiti wa kitongoji na vijiji wafanye ziara za kuelezea utekelezaji wa ilani na kutimiza wajibu wao ili kukiweka chama sehemu nzuri uchaguzi serikali za mitaa 2019.

Hakusita kukemea makundi ambayo kwa upande mwingine yanasababisha migongano baina ya wanachama na kusababisha kukiyumbisha chama. 
Aliwaasa viongozi na wanaCCM kujenga umoja,upendo,mshikamano ili kukiimarisha chama hicho. 

Awali akirudisha kadi ya CHADEMA, Ndembo alimpongeza na kumwagia sifa Rais dk. John Magufuli kwa kuitendea haki ilani ya chama kivitendo. 
"Vyama vya upinzani vilikuwa vikihitaji utatuzi wa kero na changamoto, sasa Tanzania inaneemeka, uchumi unapanda siku hadi siku, kutokana na hayo ni vema nije CCM ,kwakuwa kule nilipotoka hakuna jipya "alifafanua Ndembo. 

Nae mwenezi wa CCM Bagamoyo ,John Francis Bolizozo alisema tukielekea katika chaguzi mbalimbali zijazo, wamejipanga kushinda kwa kishindo uchaguzi wa serikali ya mitaa na hatimae madiwani na urais 2020.

Katika maadhimisho hayo kiwilaya waliweza kujitolea nguvu kazi kwenye ujenzi unaoendelea shule ya sekondari Pera na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM Pingo .
Mwenyekiti wa CCM Bagamoyo, Abdulsharif Zahoro (kulia) akimpatia kadi ya CCM, katibu wa CHADEMA kata ya Pera, Shawali Ndembo ambae amekihama chama hicho na kujiunga na CCM, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 42 ya CCM wilaya ya Bagamoyo, yaliyofanyika Pingo kata ya Pera.(picha na Mwamvua Mwinyi) 
Mwenyekiti wa CCM Bagamoyo, Abdulsharif Zahoro akimvisha fulana ambayo ni sare ya chama cha mapinduzi, katibu wa CHADEMA kata ya Pera, Shawali Ndembo ambae amekihama chama hicho na kujiunga na CCM, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 42 ya CCM wilaya ya Bagamoyo, yaliyofanyika Pingo kata ya Pera.(picha na Mwamvua Mwinyi) 


Hivyo makala CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA

yaani makala yote CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/ccm-bagamoyo-yapokea-wapinzani-watano.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA"

Post a Comment

Loading...