Loading...
title : Chongolo atangaza vita dhidi ya Magendo Kinondoni
link : Chongolo atangaza vita dhidi ya Magendo Kinondoni
Chongolo atangaza vita dhidi ya Magendo Kinondoni
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akikagua ujenzi wa Hospitali ya Mabwepande, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali wilayani humo, jana.Muonekano wa Hospitali ya Mabwepande.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (wa pili kulia) akisikiliza kero za wananchi, katika mkutano uliofanyika Zahanati ya Mpiji, Kata ya Mbweni wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali wilayani humo, kusikiliza na kutatua kero za wananchi, jana.
4.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kulia) akitoa amri ya kuwatimua askri wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokuwa wakijenga majengo katika mradi wa Shule ya Msingi, Teta, Kata ya Mbweni, kwa madai kuwa ni wazembe na walikaidi amri yake ya kuwataka kuongeza kasi yaujenzi wa bweni ili shule hiyo ifunguliwe, katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali , kusikiliza na kutatua kero za wananchi.ASkari hao walipewa saa 24 kubeba virago vyao na kuondoka katika eneo la mradi hu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kushoto) akikagua ujenzi wa Barabara ya Kilongawima, Kunduchi wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali wilayani humo, jana.DC hakuridhishwa na ujenzi wa segemu mbalimbali za barabara hiyo ukiwemo wa daraja na kutokuwepo kwa sehemu za watembea kwa miguu.
Mwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo ametangaza kuanza vita kali dhidi ya biashara halamu ya magendo, mihadarati na operesheni funga bandari bubu.
Akizungumza katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo, wilyani humo, Dar es Salaam, jana, Chongolo alisema, wanaojihusisha na biashara hizo kiama chao kimewadia na amefanya uchunguzi wa kina katika hilo.
“Mnao jihusisha na biashara ya magendo, kupitisha bidhaa katika bandari bubu mtafute kazi nyingine.Ninawafahamu na nimefuatilia kikamilifu hususan katika Kata ya Mbweni. Nitawakamata.Muda wowote operesheni kubwa itafanyika.Muache mara moja,”alisema
Chongolo wakati akihutubia wananchi katika eneo la Zahanati ya Mpiji , Mbweni.
Alisema, Mbweni ni moja ya kata ambazo zimebainika baadhi ya wananchi kujihusisha na biashara halamu ya magendo, kupitia bandari bubu.
“Najua kila kitu kinachofanyika.Tafuteni kazi zingine halali la sivyo mtaishia katika gereza langu la Boko.Haiwezekani tunahangaika kujenga uchumi kwa kukusanya kodi lakini nyie mnahujumu uchumi kwa kufanya magendo.Muda wowote nitaanza msako mkali wawahusika,”alionya mkuu huyo wa wilaya.
Katika ziara hiyo, Chongolo alikagua miradi ya barabara, maji, shule, masoko, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambapo pia aliahidi kuchangia mifuko 100 ya saruji na mabati ya kuenzeka vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Madale, ambapo vyumba hivyo vinajengwa kwa nguvu za wananchi.
Hivyo makala Chongolo atangaza vita dhidi ya Magendo Kinondoni
yaani makala yote Chongolo atangaza vita dhidi ya Magendo Kinondoni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Chongolo atangaza vita dhidi ya Magendo Kinondoni mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/chongolo-atangaza-vita-dhidi-ya-magendo.html
0 Response to "Chongolo atangaza vita dhidi ya Magendo Kinondoni"
Post a Comment