Loading...

Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China

Loading...
Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China
link : Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China

soma pia


Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China


Mheshimiwa Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, leo tarehe 13 Machi, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa WANG Ke, Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China.

Mheshimiwa WANG Ke pamoja na masuala mengine amewasilisha kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki barua ya pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China kufuatia Prof. Kabudi kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Aidha Prof. Kabudi kupitia kwa Mheshimwa Balozi ameshukuru kwa salamu hizo za pongezi alizopokea.

Katika mazungumzo yao, Prof. Kabudi na Balozi WANG Ke, wameahidi kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizo mbili. Na kwa pamoja wamesisitiza umuhimu wa kuendelea na jitihada za kuimarisha mahusiano ya kisiasa, kijamii, kiuchumi hususan kwenye maeneo la uwekezaji, biashara, utalii na miundombinu.
                                                                      
Prof. Kabudi ametumia fursa hiyo kuishukuru Jamhuri ya Watu wa China kwa misaada ya kimaendeleo wanayoendelea kuitoa na kwamba Serikali inafurahishwa na Jinsi China inavyounga mkono jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo na kujenga uchumi.

Tanzania na China zimekuwa na mahusiano ya kidiplomasia tangu mwaka 1964 na mwaka huu zinatarajia kuadhimisha miaka 55 ya ushirikiano huo.

Mheshimiwa Wang amekuwa Balozi wa kwanza kuonana na Mhe. Kabudi tangu kuteuliwa kwake na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuiongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
13 Machi 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akipokea barua ya pongezi kutoka kwa Balozi wa China nchini, Mhe. WANG Ke. Balozi wa China aliwasilisha barua hiyo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. WANG Yi ambapo anampongeza Prof. Kabudi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mhe. Prof. Kabudi akisoma barua ya pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambayo iliwasilishwa wizarani na Balozi wa China nchini.

Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China mara baada ya kupokea barua ya pongezi.


Hivyo makala Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China

yaani makala yote Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/prof-kabudi-apokea-salamu-za-pongezi_13.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China"

Post a Comment

Loading...