Loading...
title : CUF YATEUWA WAJUMBE WAPYA TISA BODI YA WADHAMINI.
link : CUF YATEUWA WAJUMBE WAPYA TISA BODI YA WADHAMINI.
CUF YATEUWA WAJUMBE WAPYA TISA BODI YA WADHAMINI.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Baraza Kuu Taifa Chama cha Wananchi (CUF) kimeteuwa wajumbe wapya tisa wa bodi ya wadhamini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kuwa kupitia kikao cha baraza Kuu la Uongozi Taifa kilichofanyika Februari I9 mwaka huu wameweza kuteuwa wajumbe wa bodi.
Profesa Lipumba amesema kuwa wajumbe walioteuliwa na baraza kuu kutoka Tanzania bara ni Peter Malebo, Abdul Magomba, Hajira Silia, Amina Mshamu pamoja na Aziz Daghesh.
Amesema kutoka Zanzibar ni Salha Mohamed, Asha Suleiman, Suleiman Issa na Mussa Kombo.
Profesa Lipumba amefafanua kuwa baada ya kukamilisha uteuzi huo, Kaimu Katibu wa CUF tayari amewasilisha barua ya maombi ya kusajili Bodi ya Wadhamini kwa Afisa Mtendaji Mkuu RITA, huku akiambatanisha na fomu husika ya kumbukumbu za kikao cha baraza kuu kilichofanya uteuzi.
"Nakala ya barua na kumbukumbu za kikao zimewasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa" amesema Profesa Lipumba.
Katika hatua nyengine amefafanua kuwa baraza kuu limeridhia na utendaji wa bodi iliyoteuliwa machi 20I7 na kushauri majina wa wajumbe hao yapendekezwe.
Hata hivyo hivi karibuni Mahakama Kuu nchini Tanzania imetoa uamuzi wa kesi kuhusu mvutano wa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama Cha Wananchi (CUF), ikiwakataa wajumbe wapya waliokuwa wameteuliwa na timu Lipumba [Profesa Ibrahim] na timu Seif [Maalim Sharif Hamad].
Kupitia hukumu yake iliyosomwa jijini Dar es Salaam, Mahakama Kuu imeeleza kuwa wajumbe wa pande zote mbili hawakukidhi vigezo vya kuwa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, hivyo uteuzi wao umetenguliwa.
Hivyo makala CUF YATEUWA WAJUMBE WAPYA TISA BODI YA WADHAMINI.
yaani makala yote CUF YATEUWA WAJUMBE WAPYA TISA BODI YA WADHAMINI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CUF YATEUWA WAJUMBE WAPYA TISA BODI YA WADHAMINI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/cuf-yateuwa-wajumbe-wapya-tisa-bodi-ya.html
0 Response to "CUF YATEUWA WAJUMBE WAPYA TISA BODI YA WADHAMINI."
Post a Comment