Loading...

IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA

Loading...
IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA
link : IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA

soma pia


IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA

NA OWM (KVAU) - KONGWA

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa ameridhishwa na utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu katika Wilaya ya Kongwa.

Hayo ameyasema wakati wa ziara yake katika wilaya hiyo kuangalia hali ya utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.

Akitoa pongezi hizo, Naibu Waziri, Ikupa alisema kuwa ushirikishwaji wa kundi hilo maalum ni jambo la msingi katika kuhakikisha haliachwi nyuma kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo.“Endeleeni kuwajali na kuweka mipango thabiti yenye kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki sawa kama wengine,” alisema Ikupa. 

Pia, aliipongeza wilaya ya kongwa kwa kusaidia Watu wenye Ulemavu kuhudhuria maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa yanayofanyika hapa nchini.
“Matukio hayo yamekuwa yakiwapa hamasa kubwa na kuona fursa ambazo zinaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi,” alieleza Ikupa

Aidha, Mhe. Ikupa alitoa rai kwa Watu wenye Ulemavu kuwa wabunifu na kuweza kutambua fursa kutokana na mazingira waliyopo na kuzitumia kujiongezea kipato.

Hata hivyo, Naibu Waziri Ikupa alihimiza uboreshwaji wa miundombinu rafiki zitakazowesha kundi hilo, kuelimisha jamii juu ya haki za watu wenye ulemavu, uundwaji wa kamati za kuhudumia kundi hilo maalum na kuwapatia taarifa watu wenye ulemavu kuhusu fursa za mikopo zinazotolewa na halmashauri, ajira na upatikanaji wa dawa, mafuta ya wenye ualbino na vifaa saidizi. 

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi alimshukuru Mhe. Ikupa kwa kufanya ziara Wilayani humo, na kuahidi kuendelea kutoa huduma kwa kundi hilo maalum ikiwemo asilimia 2 ya mapato ya ndani ya halmashauri zinatengwa na kutoa mikopo kwa Vikundi vya Watu wenye Ulemavu, pia kuhakikisha kamati za Watu wenye Ulemavu zinaundwa katika kila Kijiji na kufanya kazi kulingana na miongozo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri, Ikupa alitembelea Kituo cha Utengamao kilichopo Mlali na Shule maalum Kongwa Kitengo cha Viziwi. Pia alitembelea Wilaya ya Mpwapwa, Shule ya msingi Chazungwa na Mpwapwa Sekondari ambazo zina wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (wa kwanza kutoka kulia) akizungumza kuhusu masuala ya Watu wenye Ulemavu alipofanya ziara Wilaya ya Kongwa kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa.
Mwalimu wa Shule ya msingi Kongwa, Kitengo Maalum cha Viziwi, Bi. Anitha Massawe akiwafafanulia wanafunzi wenye uziwi kwa lugha ya alama maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) alipotembelea shule hiyo.
Daktari wa Mazoezi ya Viungo kutoka Kituo cha Utengamao Mlali, Dkt. Nshashuku Joseph akimwelezea Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa aina ya mazoezi wanayoyatoa kwa Watoto wenye ulemavu wa viungo. (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi.
Baadhi ya wazazi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) alipotembelea Kituo cha Utengamano kilichopo Mlali, Wilaya ya Kongwa.


Hivyo makala IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA

yaani makala yote IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/ikupa-aridhishwa-na-utekelezaji-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA"

Post a Comment

Loading...