Loading...
title : KUMBILAMOTO, ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII KUHUSU WAJANE NA WALEMAVU.
link : KUMBILAMOTO, ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII KUHUSU WAJANE NA WALEMAVU.
KUMBILAMOTO, ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII KUHUSU WAJANE NA WALEMAVU.
Na. John Luhende
Mwamba wa habari
Wajane na waleva waishio kata ya Vingunguti Manispaa ya Ilala , wametakiwa kuwa na umoja na ushirikiano ilikuweza kufanya biashara ndogondogo zitakazo wasaidia kukidhi mahitaji yao ya kila siku na kumudo kurejesha fedha za mikopo ambayo wanatarajiwa kukopeshwa na Manispaa.
Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Vingunguti ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbila moto wakati wa mafunzo mafupi ya ujasilia mali yaliyofanyika chini ya Maafisa mikopo na Afisa vijana wa Manispaa ya Ilala , ambapo pia amegawa Mikate 400, kwa makundi hayo.
Aidha kumbilamoto ameitaka jamii kuto yanyanyapaa makundi hayo kwakuwa kufanya hivyo ni kinyume na agizo la Mwenyezi Mungu.
“Makundi ya yatima wajane na walemavu alisisitiza sana Mwenyezi Mungu tuyatazama sana kwa jicho la huruma na kuya saidia hivyo nawaomba sana viongozi wenzangu kwa hali na mali tujitolee misaada , nashukuru pia kama manispaa tumetenga takribani million 700 kwaajili ya mikopo “Alisema Kumbilamoto.
Mwamba wa habari pia imezungumza na Makundi yote yaliyo hudhuria mafunzo hayo ambapo Ester Toi Nzigo, ambaye anatoka kundi la Mama wajane amesema mikopo hiyo itawasaidi kwakuwa ninafuu kuliko hapa awali ambao mikopo hiyo ilikuwa inatolewa kwa Riba kubwa .
“Tuta mudu kulipa mikopo hii kwa kuwa tumesha zoea kulipa mikopo riba tutapata unafuu mkubwa tuna mshukuru sana Diwani wetu Kumbilamoto ,Rais Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia, alituahidi kuwa wananawake tutapewa mikopo sasa yametimia “Alisema
“Sisi walemavu mikopo hii itawasaidia kuondokana na hali ya kuomba omba mitaani sasa tutakuwa na biashara zetu “Alisema Fides Mwakilema .
Hivyo makala KUMBILAMOTO, ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII KUHUSU WAJANE NA WALEMAVU.
yaani makala yote KUMBILAMOTO, ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII KUHUSU WAJANE NA WALEMAVU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUMBILAMOTO, ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII KUHUSU WAJANE NA WALEMAVU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/kumbilamoto-atoa-ujumbe-mzito-kwa-jamii.html
0 Response to "KUMBILAMOTO, ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII KUHUSU WAJANE NA WALEMAVU."
Post a Comment