Loading...

MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI NCHINI KENYA WAPATIKANA NA HATIA YA MAUAJI YA BABY PENDO

Loading...
MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI NCHINI KENYA WAPATIKANA NA HATIA YA MAUAJI YA BABY PENDO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI NCHINI KENYA WAPATIKANA NA HATIA YA MAUAJI YA BABY PENDO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI NCHINI KENYA WAPATIKANA NA HATIA YA MAUAJI YA BABY PENDO
link : MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI NCHINI KENYA WAPATIKANA NA HATIA YA MAUAJI YA BABY PENDO

soma pia


MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI NCHINI KENYA WAPATIKANA NA HATIA YA MAUAJI YA BABY PENDO

MAOFISA watano wa Jeshi la Polisi walioongoza operesheni ya 2017 ambapo mtoto kwa jina baby Pendo aliuawa katika Mji wa Nyalenda kaunti ya Kisumu wamepatikana na hatia ya kifo chake. Uchunguzi ulioongozwa na hakimu mwandamizi Beryl Omollo ulitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi mjini Kisumu.Makamanda hao ni Linah Kosgei, Benjamin Koima, Christopehr Mutune Maweu, Titus Yoma na John Thiringi.

Shirika la Habari la Uingereza limesema leo kuwa wakati wa operesheni hiyo iliokumbwa na utata Bwana Yoma alikuwa Kamanda wa polisi wa kaunti ya Kisumu, Bwana Maweu alikuwa OSPD wa Kisumu Mashariki, bwana Thiringi alikuwa OSC wa kisumu ya kati huku Koima akisimamia Kisumu magharibi huku naye bi Kosgei akiongoza kituo ha polisi cha Nyalenda. Mtoto huyo aliyekuwa na miezi sita aliuawa ndani ya nyumba ya babake na maafisa wa polisi wa kitengo cha kukabiliana na ghasia ambao walikuwa wakijaribu kuzima maandamno yalioanza kufuatia matokeo ya uchaguzi wa 2017.

Katika uamuzi wake , hakimu huyo pia alimuagiza Mkurugenzi wa mashtaka Noordin Haji kuwachunguza maofisa 31 wa kikosi cha GSU ambao aliwataja kuwa 'washukiwa muhimu'. Pia maofisa wengine 20 wa polisi ambao walikuwa chini ya usimamizi wa Kosgei mjini Nyalenda pia watachunguzwa mahakama hiyo iliamuru. Wakati huo huo wazazi wake Bwana Joseph Abanja na mkewe Lencer Achieng, walisema kuwa walikuwa wakiomba maajabu ya Valentines na ni hicho walichopata na wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo maofisa hao(Makamanda hao walilaumiana huku hakuna hata mmoja akitaka kuchukuwa lawama.

Imeelezwa kuwa Baby pendo alifariki Agosti 2017, baada ya kudaiwa kupigwa katika kichwa na maofisa wa polisi kutokana na ghasia zilizokumba kaunti ya Kisumu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais. Maofisa wa Polisi walishutumiwa kwa kuvunja na kuingia katika nyumba ya Bw. Abinja katika mtaa wa mabanda wa Nyalenda.Mtoto huyo alifairiki siku tatu baadaye wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan.CHANZO BBC.


Hivyo makala MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI NCHINI KENYA WAPATIKANA NA HATIA YA MAUAJI YA BABY PENDO

yaani makala yote MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI NCHINI KENYA WAPATIKANA NA HATIA YA MAUAJI YA BABY PENDO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI NCHINI KENYA WAPATIKANA NA HATIA YA MAUAJI YA BABY PENDO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/maofisa-watano-wa-jeshi-la-polisi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI NCHINI KENYA WAPATIKANA NA HATIA YA MAUAJI YA BABY PENDO"

Post a Comment

Loading...