Loading...

Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya

Loading...
Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya
link : Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya

soma pia


Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii. 

JUMLA  ya Mashahidi 54 na vielelezo 218 vinatarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi, katika kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA), Harry Kitillya na wenzake wanne kwa ajili ya kwenda kuanza kusikilizwa.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni  Maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, Kamishna wa Sera ya uchambuzi wa Madeni kutoka Wizara Fedha na Mipango, Bedason Shallanda na msaidizi wake Alfred Misana ambapo wote wanakabiliwa na mashtaka 58 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Hatua hiyo imekuja huku tayari Kitilya na wenzake wawili Shoe na Sioi wakiwa wamekaa gerezani kwa takribani miaka mitatu ambapo walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Aprili 16, 2016. Kesi hiyo imehamishiwa Katika mahakama ya mafisadi leo Februari 12, 2019 mara baada ya washtakiwa kusomewa upya mashtaka yao na kutajiwa Idadi ya mashahidi na vielelezo vitakavyowasilishwa wakati wa ushahidi. 

Baada ya kusomewa maelezo hayo,  Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi aliwauliza washtakiwa kama walikuwa na lolote la kuongeza ambapo wote walidai kuwa hawana cha kuongeza. Kufuatia hayo,  mahakama hiyo imetoa amri ya kuhamishia shauri hilo Mahakama Kuu Kitengo cha mafisadi.

Wakati watuhumiwa wakisomewa maelezo hayo ya mashahidi (Commital) upande wa mashtaka uliwasilishwa na jopo la mawakili watatu, walii wakiongozwa na Wakili Mkuu wa serikali,  Fredrick Manyanda,  wakili wa serikali Mkuu Tumaini Kweka na wakili wa serikali George Barasa.
Aidha upande wa utetezi uliwasilishwa na jopo la mawakili  watatu wakiongozwa na Cuthbert Tenga akisaidiana na Alex Mgongolwa pamoja na Majura Magafu. Miongoni mwa mashahidi wanaotarajiwa kuitwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, aliyekuwa mwanasheria Mkuu Wa Serikali, Fredrick Welema.

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kughushi, moja la kuongoza uhalifu,  49 utakatishaji fedha, mawili ya kutoa nyaraka za uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanyanyifu moja na shtaka moja la kutoa nyaraka kwa nia ya kumdanganya kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango. 

Wanadaiwa  kati ya Machi 15, 2013 na Januari 10, 2014 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kudanyanya washtakiwa wote walijipatia Dola za Kimarekani Milioni sita wakionesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji wa upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd. 


Hivyo makala Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya

yaani makala yote Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/mashahidi-54-na-vielelezo-218.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya"

Post a Comment

Loading...