Loading...

MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA

Loading...
MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA
link : MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA

soma pia


MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA

Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akilikagua jengo jipya la Wizara yake linalojengwa katika Mji wa Serikali, Ihumwa, jijini Dodoma, wakati alipofanya ziara katika eneo hilo leo, kwa lengo la kukagua ujenzi unavyoendelea. Meja Jenerali Kingu amemtaka Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari awe amemkabidhi jengo hilo.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza na Wakandarasi wa Ujenzi wa Jengo jipya la Wizara yake, Mshauri Mwelekezi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), pamoja na wawakilishi wa Wizara yake wanaosimamia ujenzi unaoendelea wa jengo hilo katika Mji wa Serikali, Ihumwa, jijini Dodoma. Kingu amemtaka Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari awe amemkabidhi jengo hilo.

Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Aron Lunyungu, akionyesha madirisha ambayo yapo tayari kwa ajili ya kufungwa katika jengo hilo la Wizara. Lunyungu ambaye pia ndiyo Mkandarasi wa Ujezni huo ameagizwa awe amemaliza ujenzi wa jengo hilo na kumkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mwezi huu wa Februari.

……………………

Na Felix Mwagara, MOHA.

KATIBU Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, amemtaka Mkandarasi anaejenga Jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma, afanye kazi usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari awe amemkabidhi jengo hilo.

Meja Jenerali Kingu amesema kasi ya ujenzi huo umenza kusuasua kwasababu Wizara yake ilifikia hatua kubwa lakini sasa imepitwa na baadhi ya Wizara kutokana na Mkandarasi anayejenga jengo hilo kupunguza kasi ikiwa ni tofauti na ile walioanza nayo awali.

Katibu Mkuu aliyazungumza hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo la ujenzi, jijini humo, leo, na alifanya ukaguzi na baadaye alizungumza na wadau kutoka pande tatu zinazoshirikiana katika kufanikisha ujenzi huo ambao ulianza mwezi Desemba mwaka jana.

Wadau wa pande tatu wanaofanikisha ujenzi huo ni Mmiliki wa Jengo hilo ambaye ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mshauri Mwelekezi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) pamoja na Mkandarasi ambaye ni Jeshi la Magereza.

“Nimepokea taarifa ya ujenzi unaoendelea, lakini sijaridhishwa nayo kutokana na asilimia ya ujenzi huu ulipofikia mpaka sasa, mmenipa ratiba mpya ya kukamilika kwa jengo hili, kasi yenu imekua ndogo mpaka tumeanza kupitwa na baadhi ya Wizara ambazo sisi tulikua tunaongoza, sasa nataka mfanye kazi hii usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari ujenzi huu uwe umekamilika na mnikabidhi jengo hili,” alisema Meja Jenerali Kingu.

Kwa upande wake Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka TBA, Arch. Hassan Mnandala alimwambia Katibu Mkuu huyo kuwa, ataendelea kusimamia na kushauri ili Mkandarasi awe amemaliza kazi hiyo kwa wakati kama ratiba ilivyopangwa.

Naye Mkandarasi wa ujenzi huo, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Aron Lunyungu, kwa upande wake amesema ujenzi huo unaendelea na tayari ujenzi wa kuta umefanyika, na imefikia usawa wa kupaua na tayari upigaji wa ripu ndani ya jengo hilo umefanyika.

“Tunamshukuru Katibu Mkuu Meja Jenerali Kingu, leo katutembelea na ametuagiza tujipange ili tuweze kukamilisha kwa wakati ujenzi wa jengo hili, nasi tumejipanga kazi tutaifanya usiku na mchana kuhakikisha jengo hili tunalikamilisha na tunalikabidhi kwa wakati,” alisema ACP Lunyungu.


Hivyo makala MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA

yaani makala yote MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/meja-jenerali-kingu-akasirika-spidi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA"

Post a Comment

Loading...