Loading...

Mfumuko wa Bei Waendelea Kushuka hadi asilimia 3.0 Mwezi Januari 2019

Loading...
Mfumuko wa Bei Waendelea Kushuka hadi asilimia 3.0 Mwezi Januari 2019 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mfumuko wa Bei Waendelea Kushuka hadi asilimia 3.0 Mwezi Januari 2019, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mfumuko wa Bei Waendelea Kushuka hadi asilimia 3.0 Mwezi Januari 2019
link : Mfumuko wa Bei Waendelea Kushuka hadi asilimia 3.0 Mwezi Januari 2019

soma pia


Mfumuko wa Bei Waendelea Kushuka hadi asilimia 3.0 Mwezi Januari 2019

Na; Frank Mvungi- MAELEZO

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Januari, 2019 umeshuka hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 3.3 ya mwezi Desemba mwaka 2018.

Akizungumza wakati akiwasilisha hali ya mfumuko wa bei leo Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Sensa ya Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo, amesema kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Januari, 2019 umepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwezi Desemba, 2018.

“Kupungua kwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Januari 2019 kunatokana kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula katika mwezi huo ikilinganishwa na bei za mwezi Januari 2018.” alisisitiza Kwesigabo

Akifafanua, Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Januari umeendelea kupungua hadi kufikia asilimia 0.7 kutoka asilimia 1.0 iliyokuwa mwezi Desemba, 2018.

Aliongeza kuwa baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2019 ni pamoja na mchele asilimia 3.9, mahindi13.9, unga wa mahindi 8.9, mtama 5.1, unga wa muhogo 6.8, maharage 4.2, choroko 10.5, mihogo mibichi 5.6, viazi vitamu kwa asilimia 3.3, magimbi 18.6 na ndizi za kupika 13.3

Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki, mfumuko wa bei nchini Kenya umepungua hadi asilimia 4.70 kutoka asilimia 5.71 kwa mwezi Desemba 2018, nchini Uganda mfumuko wa bei kwa mwezi Januari umeongezeka hadi asilimia 2.7 kutoka asilimia 2.2 kwa ya mwezi Desemba 2018.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na kupewa majukumu ya kutoa, kusimamia, na kuratibu upatikanaji wa Takwimu rasmi nchini ikiwa ni pamoja na takwimu za mfumuko wa bei kwa ajili ya matumizi ya Serikali na wadau wa takwimu.
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akisisitiza kuhusu kushuka kwa mfumuko wa Bei hadi asilimia 3.0 kwa mwezi Januari 2019 ikilinganishwa na asilimia 3.3 kwa mwezi Desemba 2018.



Hivyo makala Mfumuko wa Bei Waendelea Kushuka hadi asilimia 3.0 Mwezi Januari 2019

yaani makala yote Mfumuko wa Bei Waendelea Kushuka hadi asilimia 3.0 Mwezi Januari 2019 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mfumuko wa Bei Waendelea Kushuka hadi asilimia 3.0 Mwezi Januari 2019 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/mfumuko-wa-bei-waendelea-kushuka-hadi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mfumuko wa Bei Waendelea Kushuka hadi asilimia 3.0 Mwezi Januari 2019"

Post a Comment

Loading...