Loading...
title : Mratibu wa Ilala Heri Shaban azawadiwa kiwanja.
link : Mratibu wa Ilala Heri Shaban azawadiwa kiwanja.
Mratibu wa Ilala Heri Shaban azawadiwa kiwanja.
Mratibu wa Umoja wa Ilala Heri Shaban akiwa na jembe begani mara baada kuzawadiwa Kiwanja kwa ufanyaji wa kazi nzuri na kuitangaza Manisipaa ya Ilala (Kulia) Mbunge Angelina Malembeka aliyetoa kiwanja hicho kumpa shaaban, Shaaban anaendesha Gruop la Ilala yetu kwa ajili ya kusikiliza kero za Wananchi na kuziwashirisha kwa watendaji wa Serikali kwa ajili ya kutatuliwa (PICHA NA EVELN MWAKATUMA)
Mbunge wa Mkoa kaskazini Unguja Angelina Malembeka (kulia) akimkabidhi Kiwanja kwa ajili ya makazi Mratibu wa Umoja wa Ilala Heri Shaban Kiwanja hicho kipo eneo la Tarafa ya Makotopola Jijini la Dodoma (PICHA NA EVELN MWAKATUMA)
Na Eveln Mwakatuma
Mratibu wa Umoja wa
Ilala yetu Heri Shaban amekabidhiwa tuzo ya Kiwanja kwa utendaji wake wa kazi vizuri na kutatua Kero za Wananchi kwa kupokea malalamiko ya Wilaya ya Ilala.
Tuzo hiyo ya Kiwanja alikabidhiwa na Mbunge wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Angelina Malembeka jiji la Dodoma kata ya Veyula Tarafa ya Makutopola ili ajenge nyumba ya kuishi na familia.
Akizungumza Dodoma tarafa ya Makotopola mara baada ya kumkabidhi Kiwanja Shaban, Mbunge Malembeka alisema yeye ni Mwana Ilala alikuwa akifatilia kwa karibu utendaji wa kazi wa Heri Shaban jinsi anavyopokea kero za Wananchi na kuwasilisha viongozi Kwa Watendaji wa Manispaa ya Ilala kwa ajili ya utatuzi Mara moja
"Nimetoa tuzo hii ya Kiwanja kama sehemu ya motisha kwa HERI SHAABAN kujitolea kufanya kazi yake ambayo amebuni Mpango wa kusikiliza hizo kero kila siku kupitia Wasap na mara baada Mwananchi kuwasilisha Kero inapelekwa kwa wahusika kwa ajili ya utatuzi ".Alisema Malembeka.
Malembeka alisema kupitia gruop hilo amekuwa akisoma kila siku Kero ambazo zinapokelewa za Wananchi zinapata majibu Kwa wakati.
Malembeka amewataka vijana wengine kubuni Mpango huo kama aliobuni Shaban ili kusaidiana na Serikali kutatua Kero mbalimbali kwa ajili ya kuleta Maendeleo.
"Heri Shaban sijamfahamu leo nimemfahamu mda Mirefu toka mwaka 2000 nikiwa Diwani wa Chanika na Diwani wa Msongola 2005 Pia nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati za huduma ya Jamii Manispaa Ilala Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala Tabu Shaibu alinikabidhi wakati huo kufanya naye kazi kwa ajili ya kutangaza kazi za Madiwani wa Manispaa ya Ilala na kuitangaza Manisipaa Ilala "alisema.
Amemtaka shaban kuendelea na Mpango huo uwe endelevu kila siku kwani chombo alichobuni watu wanawasilisha Kero ni cha mfano.
Naye Mratibu Heri Shaban mara baada kupokea eneo hilo la Kiwanja alishukuru kwa Mbunge Malembeka kumthamini pale alipotoa Mwenyezi Mungu aweze kumzidishia.
Shabani alisema anatarajia kuanza ujenzi hivi karibuni kwa ajili ya kujenga nyumba ya kuishi .
"mpaka sasa nimeshachangiwa shilingi 600,000 ya kuanza ujenzi wa nyumba, pesa hizo nimechangiwa na baadhi ya viongozi wa Manispaa ya Ilala wamemunga mkono mbunge mara baada kunipa kiwanja mmoja amechangia mifuko mitano ya saruji na wawili kila mmoja wamenipa mifuko kumi kumi ya saruji
Sawa na fedha kashi 600,000 nashukuru mwaka huu nimeanza vizuri "alisema Shaaban
Akielezea Mikakati yake kwa Mwaka 2019 Shaaban alisema katika Mwaka huu 2019 anatarajia kupokea Kero nyingi kwa kushirikiana na watendaji wa Serikali atazifikisha kwa wakati ili wana Ilala waweze kupata huduma bora kwa ajili ya kukuza Maendeleo "alisema Shaaban
Alisema katika mwaka huu Mikakati aliyojiwekea kuanzisha vikundi vya Wanawake Wilaya ya Ilala vitavyoshirikiana na Serikali katika kukuza Maendeleo na uchumi wa viwanda pamoja na kuitangaza Ilala.
Hivyo makala Mratibu wa Ilala Heri Shaban azawadiwa kiwanja.
yaani makala yote Mratibu wa Ilala Heri Shaban azawadiwa kiwanja. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mratibu wa Ilala Heri Shaban azawadiwa kiwanja. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/mratibu-wa-ilala-heri-shaban-azawadiwa.html
0 Response to "Mratibu wa Ilala Heri Shaban azawadiwa kiwanja."
Post a Comment