Loading...

MUUGUZI ASIMAMISHWA KUTOA HUDUMA

Loading...
MUUGUZI ASIMAMISHWA KUTOA HUDUMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MUUGUZI ASIMAMISHWA KUTOA HUDUMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MUUGUZI ASIMAMISHWA KUTOA HUDUMA
link : MUUGUZI ASIMAMISHWA KUTOA HUDUMA

soma pia


MUUGUZI ASIMAMISHWA KUTOA HUDUMA

BARAZA LA UUGUZI NA UKUNGA LA MSIMAMISHA AFISA MUUGUZI MKUNGA MSAIDIZI MARTINI CHAMANI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MOUNT MERU ARUSHA KWA MUDA WA MWAKA MMOJA.
 
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, katika kikao chake cha 196 limemsimamisha Muuguzi Martin Chama kutoa huduma za Uuguzi na Ukunga kwa muda wa mwaka mmoja tangu tarehe 7.02.2019 baada ya kumtia hatiani na makosa mawili kati ya manne yaliyowasilishwa katika Baraza la Uuguzi na Ukunga mwezi Septemba 2018.
 
Makosa hayo ni pamoja na kufika kazini akiwa amelewa na kutaka kuhatarisha usalama wa wagonjwa na ndugu zao kwa kushindwa  kutoa huduma kwa umakini na weledi.
 
Awali ofisi ya Msajili wa baraza la Uuguzi na Ukunga lilipokea tuhuma kutoka Hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mount Meru Arusha kupitia kwa Muuguzi mkuu wa mkoa ambaye pia ni msimamizi wa maadili wa mkoa wa Arusha kwa mujibu wa sheria N0 1ya mwaka 2010.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo muuguzi huyu  alifika kazini tarehe 26.09.2018  zamu ya usiku majira ya saa tatu husiku akiwa amelewa na alianza kuwasumbua ndugu waliokuwa wakiwaangalia wagonjwa wao kutaka kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa ili hali akiwa amelewa sana hali ambayo ingesababisha kuhatarisha  maisha ya wagonjwa kwa kuwa hakuwa na umakini.
 
Tuhuma hizi ziliwasilishwa na walalamikaji wawili waliokuwa wakiuguza wagonjwa wao.
 
Ofisi ya Msajili ilituma Afisa kutoka baraza la Uuguzi na Ukunga ambaye aliungana na timu ya Mkoani Arusha ikiongozwa na Muuguzi mkuu wa Mkoa wa Arusha.Timu hii ilifanya uchunguzi wa awali na kubaini mapungufu yaliyofanywa na muuguzi huyu ambayo ni kinyume na maadili ya Uuguzi na Ukunga.
 
Taarifa hiyo ilipelekwa katika kikao cha dharura cha bodi cha 195 ambacho pamoja na mambo mengine ilijadili taarifa hii na kuamua shauri hili lisikilizwe  kataka kikao cha bodi cha 196 ambayo itahusisha mtuhumiwa na mashahidi ambao ni walalamikaji na watumishi waliokuwepo siku ya tukio.
 
Shauri hili limesikilizwa tarehe 07.02.2019 ambapo Ushahidi uliotolewa umemtia hatiani bwana Martini kwa kulewa na kushindwa kutoa huduma kwa wagonjwa kwa weledi na kutaka kuhatarisha Maisha ya wagonjwa na ndugu zao.baraza liliadhimia kwa kauli moja kumsimamisha kutoa huduma hizi kwa muda wa mwaka mmoja.
 
Baraza la Uuguzi na Ukunga ni Mamlaka iliyoanzishwa kisheria na kufanya kazi chini ya Sheria inayoitwa The Nursing and Midwifery Actof 2010.Baraza lilianzishwa kwa ajili ya kulinda umma kutokana na huduma zinazotolewa na wauguzi na wakunga nchini na linafanya kazi kwa kusimamia ubora katika mafunzo na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinazingatia viwango vilivyowekwa.
 
Imetolewa na
Agnes Mtawa
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga
09.02.2019


Hivyo makala MUUGUZI ASIMAMISHWA KUTOA HUDUMA

yaani makala yote MUUGUZI ASIMAMISHWA KUTOA HUDUMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MUUGUZI ASIMAMISHWA KUTOA HUDUMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/muuguzi-asimamishwa-kutoa-huduma.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MUUGUZI ASIMAMISHWA KUTOA HUDUMA"

Post a Comment

Loading...