Loading...

SERIKALI YAAGIZA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA MSINGI KUTUMBULIWA

Loading...
SERIKALI YAAGIZA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA MSINGI KUTUMBULIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAAGIZA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA MSINGI KUTUMBULIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAAGIZA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA MSINGI KUTUMBULIWA
link : SERIKALI YAAGIZA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA MSINGI KUTUMBULIWA

soma pia


SERIKALI YAAGIZA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA MSINGI KUTUMBULIWA

Kaimu Mrajisi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Wizara ya Kilimo Charles Malunde amewataka warajisi wa kila mkoa kuwaondoa mara moja kwenye nafasi zao viongozi wa vyama vya msingi ambao watabainika kujihusisha na ubadhirifu wa fedha za ushirika huku akibainisha kuwa muda wakupiga dili umeshapita.

Hayo ameyasema leo Februari 22,2019 Mjini Shinyanga kwenye kikao cha Wadau wa Pamba kilichofanyika kwenye ukumbi wa SHIRECU,ambacho kimejumuisha mikoa sita ukiwemo mkoawaMwanza,Geita,Simiyu,Mara,Shinyanga na Tabora ambapo amesema ushirika wa sasa siyo kama ule wa zamani wa kupiga dili na kuongeza kuwa watahakikisha kila fedha ya vyama vya msingi inatumika ipasavyo. 

  Alisema suala la uchaguzi ndani ya vyama vya ushirika halina msimu na kuwataka warajisi wasaidizi wa kila mkoa kuchukua hatua haraka, iwapo kiongozi akienda kinyume na taratibu aondolewe mara moja katika nafasi yake kwani wanahitaji kuleta mabadiliko kwenye ushirika ambao utakuwa unaweza kujitegemea.  

“Tunahitaji mtu anayeingia kwenye ushirika ajitathimini kwanza mwenyewe ,tunahitaji kujenga ushirika na mahali popote pale mkigundua kuna shida chukueni hatua,najua hata nyinyi viongozi kama mngekuwa na shida leo hii tusingekuwa nanyi hapa kwenye kikao hiki ninachowasihi simamieni vizuri ushirika”,alisema kaimu mrajisi. 

  Kwa upande wake Meneja wa Bodi ya Pamba Kanda ya Ziwa Jones Bwahama alisema changamoto kubwa waliyokumbana nayo vijijini ni baadhi ya wakulima kutonyunyizia dawa pamba yao kwa hofu kuwa itakauka kutokana na mvua kutonyesha jambo ambalo ni upotoshaji mkubwa na kuwatakakupulizia ili kuzuia wadudu wasiendelee kuharibu. 

Alisema wakulima wasipopulizia viuadudu pamba inaendelea kuharibika kwani kuna wadudu wanaofyonza na wanaokula vitumba ambapo majani yanaanza kujikunja ,ambapo aliwaondoa hofu wakulima na kuwataka kupulizia pamba yao isiendelee kuharibika kwani haiwezi kukauka. Kikao hicho cha wadau wa pamba kimejumuisha warajisi wasaidizi wa mikoa,maafisa ushirika,viongozi wa vyama vya msingi na wadau wa zao la pamba,ambao wanatoka katika mikoa sita ambayo yote inajihusisha na kilimo cha pamba licha ya mikoa kufikia kwa sasa 17 lakini kikao hicho kimehusisha mikoa sita.  Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) Luhende Richard Luhende akifungua mkutano huo wa wadau wa zao la Pamba - Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blogKaimu Mrajisi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Wizara ya Kilimo Charles Malunde akizungumza kwenye kikao hicho cha wadau wa zao la Pamba, na kuzitaka AMCOS kuacha kufanya kazi kimazoea.Wajumbe wa wakiwa kwenye mkutano.Wajumbe wakiwa kwenye mkutano wakisikiliza nasaha za viongozi.Meneja wa Bodi ya Pamba kutoka Kanda ya Ziwa Jones Bwahama akiwasilisha taarifa ya usambazaji wa Viatilivu pamoja na Maandalizi ya Msimu wa ununuzi wa Pamba katika msimu ujayo, na kuwataka wakulima wapulizie dawa na siyo kusubili hadi mvua zianze kunyesha.Nicodemas Sicilima ambaye ni meneja wa Mashirikiano wa mikoa na wilaya akiwasilisha taarifa ya mikakati ya kuendeleza zao la Pamba na vyama vya msingi vya ushirika Amcos.Anjelina Lukas ambaye ni Kaimu mafunzo kutoka chuo cha Ushirika Moshi Tawali la Kizumbi- Shinyanga, akiwasilisha mpango wa mafunzo kwa wajumbe wa Bodi na watendaji wa vyama, ili waweze kuwa na uwezo wa namna ya uandishi wa vitabu vya Amcos.Meneja wa Bank ya CRDB Tawi la Shinyanga Mjini Said Pamui akichangia mada namna taasisi hiyo ya fedha inavyoweza kushiriki kikamilifu katika kuchangia kutatua changamoto inavyovikabili vyama hivyo vya Ushirika, ikiwamo ukopeshaji wa fedha pamoja na kufungua akaunti za wakulima.Wajumbe wakiendelea na kikao.Meneja wa chama kikuu cha Ushirika Chato Joseph Masingiri akichangia mada kwenye kikao hicho.Kaimu Meneja wa chama cha ushirika Mbongwe na Bukombe Elikana Kagoma akichangia mada kwenye kikao hicho, ili kuboresha uzalishaji wa zao la Pamba.Meneja mkuu wa chama cha ushirika Igembensabo- Tabora Emmanule Malunde akichangia mada kwenye kikao hicho na kulalamikia kuwepo na baadhi ya vyama vya msingi vya Ushirika Amcos mkoani Tabora kutafuna fedha za ushuru wa zao la Pamba Milioni 122.Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoani Geita (GCU) Zainabu Shabani, akichangia mada kwenye kikao hicho na kulalamikia kuwepo na upungufu wa viatilifu vya kuulia wadudu pamoja na kutokwenda kwa wakati kwa wakulima.Joseph Mihangwa ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) naye akichangia mada kwa lengo la kuboresha zaidi kilimo cha zao hilo la Pamba.Wajumbe wakiwa mkutanoni.Mkutano ukiendelea. Wajumbe wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa mada pamoja na majibu ambayo wameuliza ili kuboresha zao hilo la Pamba.Mkutano ukiendelea.Wajumbe wakiwa mkutanoni.Awali mrajisi msaidizi kutoka mkoa wa Mwanza Saulo Paulo Lunyeka akisoma ajenda za kikao hicho cha wadau wa zao la Pamba. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog


Hivyo makala SERIKALI YAAGIZA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA MSINGI KUTUMBULIWA

yaani makala yote SERIKALI YAAGIZA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA MSINGI KUTUMBULIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAAGIZA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA MSINGI KUTUMBULIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/serikali-yaagiza-wabadhirifu-kwenye.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI YAAGIZA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA MSINGI KUTUMBULIWA"

Post a Comment

Loading...