Loading...
title : SIMBA YAPELEKA SALAMU YA KAMWENE KWA LIPULI, YASHINDA BAO 3-1
link : SIMBA YAPELEKA SALAMU YA KAMWENE KWA LIPULI, YASHINDA BAO 3-1
SIMBA YAPELEKA SALAMU YA KAMWENE KWA LIPULI, YASHINDA BAO 3-1
Na Agness Francis, blogu ya jamii.
KAMWENE Lipuli!Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara Simba SC kufanikiwa kuuvunja mwiko kwa kuwatandika Wanapaluhengo Lipuli FC mabao 3-1 katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili msimu huu 2018-19.
Mchezo huo wa Simba na Lipuli umefanyika leo Februari 26, 2019 katika dimba CCM Samora lililopo mkoani Iringa .Mchezo ulikuwa ni wa vuta ni kuvute kwa timu zote mbili. Simba walionekana kuwa na morali zaidi ya kutafuta ushindi wa alama tatu ili kujiweka mahali pazuri katika msimamo wa Ligi Kuu.Katika mchezo huo wa leo, kipindi cha kwanza dakika ya tano Simba waliandika bao la kwanza kupitia mchezaji wake mahiri Cloutus Chota Chama a.k.a Triple C.Mchezaji wa Lipuli Paul Nonga aliisawazishia timu yake dakika ya 19 .
Kabumbu liliendelea kuchezwa ambapo kila timu walikuwa wakionesha umakini na kushambuliana kwa zamu.Dakika ya 43 yule yule Cloutus Chama aliifungia tena timu yake goli la pili la kuongoza kupitia mkwaju wa penalti, mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika wachezaji wanakwenda mapumzikoni Simba walikuwa wanaongoza bao 2-1 dhidi ya Lipuli.
Kipindi cha pili cha mchezo huo kilianza kwa timu ya Simba wakiwa na kasi zaidi huku Lipuli wao walionekana kupotea mchezoni ambapo waliwapa fursa nyingine wachezaji wa Simba kuongeza goli la tatu katika dakika ya 57 ambapo mshambuliaji aliye kwenye ubora wake Medie Kagere a.k.a Mzee wa Jicho Moja kufunga.
Katika msimamo wa Ligi Kuu, Simba ikiwa nafasi ile ile ya 3 akiwa na alama 48 na michezo 19,Yanga wao wakiwa vinara wa ligi hiyo wakiwa na alama 61 michezo 25,wakifuatiwa na Azam kwenye alama 50 akiwa ameshacheza michezo 25 pia.
Simba SC
Lipuli FC
Hivyo makala SIMBA YAPELEKA SALAMU YA KAMWENE KWA LIPULI, YASHINDA BAO 3-1
yaani makala yote SIMBA YAPELEKA SALAMU YA KAMWENE KWA LIPULI, YASHINDA BAO 3-1 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIMBA YAPELEKA SALAMU YA KAMWENE KWA LIPULI, YASHINDA BAO 3-1 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/simba-yapeleka-salamu-ya-kamwene-kwa.html
0 Response to "SIMBA YAPELEKA SALAMU YA KAMWENE KWA LIPULI, YASHINDA BAO 3-1"
Post a Comment