Loading...

Tuzo 30 za Tamasha la Filamu la Kimataifa (SZIFF) kutolewa Februari 23 Mlimani City

Loading...
Tuzo 30 za Tamasha la Filamu la Kimataifa (SZIFF) kutolewa Februari 23 Mlimani City - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tuzo 30 za Tamasha la Filamu la Kimataifa (SZIFF) kutolewa Februari 23 Mlimani City, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tuzo 30 za Tamasha la Filamu la Kimataifa (SZIFF) kutolewa Februari 23 Mlimani City
link : Tuzo 30 za Tamasha la Filamu la Kimataifa (SZIFF) kutolewa Februari 23 Mlimani City

soma pia


Tuzo 30 za Tamasha la Filamu la Kimataifa (SZIFF) kutolewa Februari 23 Mlimani City




Hussein Ndubikile
Mwamba wa habari
Jumla ya Tuzo  30 za Filamu zinatarajiwa kutolewa katika Tamasha la Filamu la Kimataifa la SZIFF litatalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Februari 23 mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari leo  jijini humo Mkurugenzi Uendeshaji vipindi wa Televisheni ya Azam, Yahaya Mohamed amesema kwa takribani mwezi mmoja na nusu Chaneli ya Sinema Zetu ilionyesha filamu zote zilizopita duru la kwanza ambapo 237 zilionyeshwa zikijumuishwa filamu ndefu, fupi, tamthiliya pamoja na makala.

Ameabinisha kuwa tuzo za SZIFF zimegawanyika katiika makundi mawili zikiwemo za Swahili Panorama ikijumuisha filamu zote zilizosajiliwa moja kwa moja  katika tuzo hizo huku kundi la pili likijumuisha World Cinema zilizosajiliwa zikitumia lugha ya kigeni zikiwa na tafsiri ya  Kiingereza hususan kwa zile ambazo hazikuandaliwa kwa lugha hiyo.
“ Tamasha la SZIFF leo linatangaza filamu zilizopita  katika mchujo wa mwanzo ili kuwania tuzo za sinema zetu kwa mwaka huu,” amesema Mohamed.
Amesisitiza kuwa katika kuhakikisha tamasha hilo linakuwa karibu na watazamaji na kupanua wigo wa ushindani miongoni mwa wasanii na wadau wa sanaa Afrika wameongeza vipengele viwili vipya kikiwemo kipengele cha Tamthiliya na World Cinema.
Amefafanua kuwa katika kipengele cha Tamthiliya tuzo zitakazoshindaniwa ni Tuzo ya Tamthiliya bora, Muongozaji bora, Mwandishi bora, Mhariri bora wa picha jongevu huku za world cinema zitakuwa ni mtunzi bora wa muziki asili pamoja na mpiga picha bora, Muigizaji bora wa kike na kiume na filamu bora.
Amesema washindi watapata zawadi kati ya Sh milioni moja hadi milioni 5 kulingana na ukubwa wa tuzo pamoja na cheti cha tuzo hizo huku akibainisha upatikanaji wa washindi wa kila kipengele watakaowania tuzo 30 umegawanyika katika sehemu mbili wakiwemo washiriki waliochaguliwa na Jopo la Majaji kwa kuzingatia vigezo na mashati na kwamba sehemu ya pili ni washiriki waliochaguliwa na watazamaji kupitia tovuti na ujumbe wa meseji.

Kwa upande wake Mratibu wa tamasha hilo, Sophia Mgaza amesema mwaka huu kumekuwa na mafanikio makubwa kwani filamu nyingi za mikoani zimeingia duru la pili tofauti na mwaka jana ambapo zilitoka Dar es Salaam.
Amezitaja miongoni mwa filamu zilizoingia duru la  pili ni Iyango, Petu na Guru, Siyabonga, Kiumeni, Mama Afrika, Dema, Safari pamoja na T-Junction.

Nyingine upande wa filamu za vichekesho ni Kazoa ndani ya Imani, Mama Mwali, Mchumia pamoja na Mwali wa Kijiji.
Sophia amesema filamu zilizoingia duru la pili zitaanza kuonyeshwa leo Saa 10 jioni katika Chaneli ya Sinema Zetu.

Naye Mwenyekiti wa Jopo la Majaji, Profesa Martin Mhando amesema upatikanaji wa washiriki katika kila kipengele umezingatia vigezo vingi na kwamba filamu zlizoshinda duru la pili ni zile zenye ubora wa hali ya juu.

Pia ameongeza kuwa mwaka uliopita Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete alikuwa mgeni wa heshima katika hafla ya tamasha hilo lililovutia wengi na kwamba kwa mwaka huu mgeni rasmi bado hajawekwa wazi.


Hivyo makala Tuzo 30 za Tamasha la Filamu la Kimataifa (SZIFF) kutolewa Februari 23 Mlimani City

yaani makala yote Tuzo 30 za Tamasha la Filamu la Kimataifa (SZIFF) kutolewa Februari 23 Mlimani City Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tuzo 30 za Tamasha la Filamu la Kimataifa (SZIFF) kutolewa Februari 23 Mlimani City mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/tuzo-30-za-tamasha-la-filamu-la.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Tuzo 30 za Tamasha la Filamu la Kimataifa (SZIFF) kutolewa Februari 23 Mlimani City"

Post a Comment

Loading...