Loading...
title : Uchomaji wa Mkaa Unaleta Athari Kubwa Kimazingira Kiuchumi na Kijamii.
link : Uchomaji wa Mkaa Unaleta Athari Kubwa Kimazingira Kiuchumi na Kijamii.
Uchomaji wa Mkaa Unaleta Athari Kubwa Kimazingira Kiuchumi na Kijamii.
Na Masanja Mabula -Pemba..27/02/2019.
ASASI isiyo ya Kiserikali ya Misitu ya Jamii Pemba (Community Forests Pemba-(CFP) , imesema suala la uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za uchomaji wa mkaa unaleta athari kubwa kimazingira , kiuchumi na kijamii.
MKurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo Mbarouk Mussa Omar amesema katika kukabiliana na hali hiyo, wameanzisha tanuri la kuchomea makaa ambalo ni rafiki wa mazingira.
Amesema kwamba kwa sasa tanuri hilo ambalo ni la majaribio linasimamia na Wizara ya Kilimo , Maliasili na Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano wa asasi hiyo.
Mbarouk amesema kuwa , Wizara ya Kilimo wanasimamia na baada ya muda watatoa tamko juu ya kuendelea kuenezwa tanuri katika maeneo mengine.
“Tanuri hii ni mkombozi wa mazingira , kwani itasaidia kuyalinda na kuhifadhi kutokana na kwamba inatumia kuni kidogo lakini kipato chake ni kikubwa”alifahamisha.
Suleiman Juma Khamis kutoka Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka Pemba , amesema iwapo wananchi watayatumia tanuri hiyo itapunguza uharibifu wa mazingira na kuilinda ardhi.
Aidha amesema tanuri hiyo inauwezo wa kudhitbi ukataji wa miti ovyo, kwani inatumia kuni kidogo kuliko kutumia tanuri za kizamani ambazo huharibu mazingira.
“ Tanuri hii pia inasaidia kuilinda ardhi kwani wanaoitumia katika tanuri za kawaida mbali na kukata miti ovyo , pia huharibu ardhi ya kilimo”alifahamisha.
Mmoja wa wadau wa mazingira Yahya Khatib Suleiman na fundi wa ujenzi wa tanuri hiyo Julius Gachiri wamesema taunuri hiyo litasaidia utunzaji wa mazingira.
Yahya amewataka wananchi hususani wachomaji wa mkaa, kuichangua fursa hiyo na kuanza maandaliz ya kujenga tanuri wakati Wizara itakapotoa maamuzi yake.
Hivyo makala Uchomaji wa Mkaa Unaleta Athari Kubwa Kimazingira Kiuchumi na Kijamii.
yaani makala yote Uchomaji wa Mkaa Unaleta Athari Kubwa Kimazingira Kiuchumi na Kijamii. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Uchomaji wa Mkaa Unaleta Athari Kubwa Kimazingira Kiuchumi na Kijamii. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/uchomaji-wa-mkaa-unaleta-athari-kubwa.html
0 Response to "Uchomaji wa Mkaa Unaleta Athari Kubwa Kimazingira Kiuchumi na Kijamii."
Post a Comment