Loading...

WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI SASA WAJA NA MBINU YA KUJIGEUZA WANAFUNZI

Loading...
WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI SASA WAJA NA MBINU YA KUJIGEUZA WANAFUNZI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI SASA WAJA NA MBINU YA KUJIGEUZA WANAFUNZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI SASA WAJA NA MBINU YA KUJIGEUZA WANAFUNZI
link : WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI SASA WAJA NA MBINU YA KUJIGEUZA WANAFUNZI

soma pia


WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI SASA WAJA NA MBINU YA KUJIGEUZA WANAFUNZI



 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah akitoa maelekezo kwa mkuu wa Polisi wilaya ya Hai,Lwelwe Mpina mara baada ya kufanikiwa kukamata watu tisa wakiwa na Dawa za Kulevya aina ya Mirungi ikiwa ndani ya Mabegi yanayotumiwa na wanafunzi kuhifadhi Daftari.
Askari Polisi wakitoa vifurushi vya Dawa za Kulevya aina ya Mirungi iliyokuwa imehifadhiwa katika mabegi yanayotumiwa na wanafunzi kuhifadhi Daftari.
Sehemu ya Dawa za kulevya aina ay Mirungi iliyokamatwa ikiwa imehifadhiwa kwenye mabegi madogo ikisafirishwa kuelekea mkoani Arusha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi Hamisi Issah akiangalia vifurushi vidogo vya Dawa za kulevya aina ya Mirungi iliyokamatwa Latina eneo la KIA Juction.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Hamisi Issah akionesha sehemu ya Dawa za kulevya aina ya Mirungi iliyokamatwa katika wilaya ya Hai ikisafirishwa kuelekea Arusha .
Baadhi ya watuhumiwa wa usafirishaji wa Dawa za kulevya  wakiwa kaaika gari la Polisi tayari kuelekea Mahakamani kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya kaskazini . 
 
WAFANYABIASHARA na Wasafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi wamekuja na mbinu nyingine mpya ya kujigeuza wanafunzi na kisha kuficha Mirungi katika mabegi madogo yanayotumiwa na wanafunzi kuhifadhi Daftari kwa lengo la kukwepa mkono wa askari Polisi.
 
Mbinu nyingine ambazo jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro imezigundua hivi karibuni ni pamoja na kutumia magari ya Kifahari yakiwemo Toyota Land Cruser ,Toyota Alphasad,Toyota Vanguard huku mbinu nyingine zikiwa ni kufanyia mabadiliko gari aina ya Toyota Noah ili kurahisisha ubebaji wa Mirungi kwa kificho.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah alisema wasafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi wameendelea kubuni mbinu kila kukicha baada ya zile za awali kushtukiwa na Polisi huku akitoa onyo kwa wamiliki wa Magari ya abiria kujiingiza katika mtego wa kusafirisha dawa hizo.
 
“Hapa kuna mizigo ambayo imekamatwa na askari wetu wakiwa barabarani ,hii ni mbinu mpya  ya usafirishaji  ,haya mabegi unayoyaoona yote ni mabegi yanayoonesha mbebaji amebeba Madaftari  anaenda shuleni ,lakini haya sio madaftari ni Mirungi ,ni mizigo iliyokamatwa kwenye mabasi tofauti tofauti”alisema Kamanda Issah. 
 
Alisema katika tukio hilo watuhumiwa tisa  wakiwemo wanawake wawili wamekamatwa wakiwa na jumla ya kilogramu 64 baada ya sakari Polisi kupekuwa magari matatu ya Abiria yaliyokuwa yakitokea  yakiendelea na safari kutokea Moshi yakielekea Arusha.
 
“Naona mbinu zinaendelea kubadilika ndani ya wiki mbili ,mbinu tatu tofauti,kwanza ya kujaza kwenye magari,pili ya kutoboa magari kabisa,tatu kama mwanafunzi  nyingine kama mtu anaenda hospitali amejifunga maplasta sasa hizi mbinu zitafika mpaka lini na sisi tunashukuru askari wangu wanafanya kazi vizuri”alisema Kamanda huyo wa  Polisi Kilimanjaro.
 
Kamanda Issah amewataja wanaoshikiliwa hadi sasa kuwa ni pamoja na  Ibrahim Masuli, Godfrey Richard, Chrispin  Baltazar, Fanuel Hamad,na Jackline Mushi huku wengine wakiwa ni Lucy Petro ,Nuru Haruna,Silvesta Fabian naMinyari Miandei.
 
Alisema kwa sasa askari polisi wameamua kupekuwa magari yote yakiwemo ya abiria huku akiwataka abiria kutoa ushirikiano kwa jeshi l a Polisi pindi wanapoona mizigo yenye mashaka ili kuwaondolea adha ya kuchelewa kufika safari zao kutokana na usumbufu watakao pata barabarani.
 
“Tunawasihi abiria maana kuna abiria wengine wakiona askari   wanapekua gari wanakasirika,msikasirike hii ndio kazi ya kupekuwa ,vinginevyo  muwe mnatuambia ndani ya gari amepanda mtu wa ajabu na amebeba madawa ya kulevya  aina ya mirungi  hapo ndio itakuwa ni nanafuu na tutafanya kazi kwa muda mfupi li muendelee  na safari “alisema Issah.
 
Kamanda Issah aliwataka wamiliki wa mabasi ya abiria kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi  ili kuhakikisha biashara hiy inakoma kwa kukataa kubeba abiria wenye mizigo ambayo wanatilia shaka na kwamba kwa kuendelea kuwabeba itapelekea kuwaingiza katika matatizo na vyombo vyao.
 
“Sasa hivi sio imekuwa ni wanafunzi ambao madaftari yao ni mirungi iliyobebwa nyuma ,kwa hali kama hiyo tunawasihi  wale wote wasafirishaji wa abiria kutokea Moshi kwenda Arusha wawe makini  utawachelewesha abiria wako,upekuzi utaendelea  na ninaelekeza askari waendelee usiku iwe mchana”alisema Issah.
 
“Kuna watu wakiona gari inapekuliwa wanatubeza ,sasa hivi tukikuona wewe unatubeza askari watakukamat,a  wanawabeza askari wanaofanya kazi yao  halafu tutakuhoji unatubeza kwa sababu gani,kwa hali kama hiyo tunaagiza askari waendelee kukamata mirungi na wasiiache”aliongeza Kamanda Issah.
 
 Kukamatwa kwa Dawa hizo  zinafanya idadi kamili ya Dawa za kulevya aina ya Mirungi zilizokamatwa katika kipindi cha wiki mbili kufikia kilogramu 564 pamoja na vyombo vya usafiri yakiwemo magari matatu na pikipiki moja.


Hivyo makala WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI SASA WAJA NA MBINU YA KUJIGEUZA WANAFUNZI

yaani makala yote WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI SASA WAJA NA MBINU YA KUJIGEUZA WANAFUNZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI SASA WAJA NA MBINU YA KUJIGEUZA WANAFUNZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/wasafirishaji-wa-mirungi-sasa-waja-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI SASA WAJA NA MBINU YA KUJIGEUZA WANAFUNZI"

Post a Comment

Loading...