Loading...

WAZIRI KANYASU AWAHAKIKISHIA WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU KUONGEZEWA MIKATABA

Loading...
WAZIRI KANYASU AWAHAKIKISHIA WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU KUONGEZEWA MIKATABA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI KANYASU AWAHAKIKISHIA WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU KUONGEZEWA MIKATABA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI KANYASU AWAHAKIKISHIA WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU KUONGEZEWA MIKATABA
link : WAZIRI KANYASU AWAHAKIKISHIA WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU KUONGEZEWA MIKATABA

soma pia


WAZIRI KANYASU AWAHAKIKISHIA WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU KUONGEZEWA MIKATABA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii. Mhe. Constantine Kanyasu amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya misitu Tanzania kuwa atashughulikia ombi lao la kutaka kuongezewa muda wa mikataba yao kutoka  miaka miwili hadi  mitano ya kupewa mgao wa vitalu vya miti

Pia ameahidi kuyafanyia kazi malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa ofisini kwake na wamiliki hao yakiwemo ya gharama za tozo ya ushuru wa mazao ya misitu  (Cess) inayotozwa na Halmashauri za wilaya ya Mufindi ambayo licha  Serikali kutoa maagizo ya kuzuia tozo hiyo bado wadau hao wanaendelea kutozwa.

 Mhe. Kanyasu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Rais wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu Tanzania (SHIVIMITA) na Wanachama wa Shirikisho hilo  waliomtembelea ofisini kwake  jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo,  Rais wa SHIVIMITA, Ben Sulus amemuomba Naibu Waziri  aangalie  namna ya kuwasaidia wadau hao waongezewe muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi mitano ya kupewa mgao wa vitalu vya misitu ili waweze kupata mikopo kutoka kwenye Taasisi za Kifedha kwa ajili ya kuendeshea viwanda vyao

Rais huyo ameeleza kuwa Taasisi za Kifedha  zimekuwa zikiwanyima  mikopo kwa kuhofia fedha zao kupotea kutokana na wadau hao kutokuwa na uhakika wa kuongezewa mikataba mara baada ya mikataba yao ya kuvuna magogo ya miaka miwili waliyopewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).

Amesema  endapo watapewa mikataba  ya miaka mitano watakuwa na uhakika wa kuweza kuendeleza viwanda vyao kwa vile Taasisi hizo za Kifedha zitaweza kuwapa mikopo watakayoomba na  zitakuwa na uhakika wa kurudishiwa  fedha hizo.

Katika hatua nyingine, Wadau hao wamemuomba awe mlezi wao katika jitihada wanazozichukua za kuhakikisha wanakuwa wazalishaji wa bidhaa za mwisho kama vile milango pamoja na meza   zitokanazo na mbao badala ya kujikita kuuza mbao tu.
 .Rais wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu Tanzania ( SHIVIMITA)  Ben Sulus akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu kuhusu kuongezewa muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi miaka mitano ya kupewa vitalu vya miti katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo mkoani Iringa wakati Washirika hao walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisalimia na baadhi yaWanachama wa Shirikisho la Viwanda vya misitu Tanzania mara baada ya kufanya mazungumzo nao kuhusu ombi la  kuongezewa muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi miaka mitano ya kupewa vitalu vya miti katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo mkoani Iringa wakati Washirika hao walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma


Hivyo makala WAZIRI KANYASU AWAHAKIKISHIA WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU KUONGEZEWA MIKATABA

yaani makala yote WAZIRI KANYASU AWAHAKIKISHIA WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU KUONGEZEWA MIKATABA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KANYASU AWAHAKIKISHIA WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU KUONGEZEWA MIKATABA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/waziri-kanyasu-awahakikishia-wamiliki.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI KANYASU AWAHAKIKISHIA WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU KUONGEZEWA MIKATABA"

Post a Comment

Loading...