Loading...
title : Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki Azungumza na Wawekezaji Kutoka Nchini Utruruki. Jijini Dodoma
link : Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki Azungumza na Wawekezaji Kutoka Nchini Utruruki. Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki Azungumza na Wawekezaji Kutoka Nchini Utruruki. Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akiongea na wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies, wakati walipofanya kikao ofisini kwake juu ya fursa na miradi ya uwekazeji nchini
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akiwasikiliza wataalamu wa masuala ya uwekezaji wa Ofisi ya waziri Mkuu wakati wa kikao na wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies (hawapo pichani), wakati walipofanya kikao ofisini kwake juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe, wakiwa katika kikao na wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies wakati walipofanya kikao juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini.
Wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies wakifuatilia kikao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki (hayupo pichani), wakati walipofanya kikao juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akimkabidhi Kitabu chenye Fursa na Miradi yenye Uhitaji Mitaji ya Uwekezaji nchini , Mwekezaji toka nchini Uturuki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya MNG Group of Companies mara baada ya kufanya kikao juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini leo, tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.
Na. Ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki amekutana na Wawekezaji kutoka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies na kufanya nao mazungumzo nao juu ya miradi waliyoonesha nia ya kuwekeza hapa nchini.
Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe, Wataalamu wa masuala ya Uwekezaji na maendeleo ya Sekta Binafsi pamoja na wataalam wa Kituo cha Uwekezaji nchini, leo mjini Dodoma, tarehe 5 Januari 2019, Waziri Kairuki amebainisha wazi kuwa nia ya serikali ya awam ya tano ni kuhakikisha uwekezaji wenye tija nchini, na kwa kuzingatia mfumo wa sera ya Ushirikiano baina ya sekta Binafsi na Umma inahakikisha inavutia wawekezaji zaidi.
“Tunazo fursa na miradi inayohitaji mitaji ya uwekezaji hapa nchini, jukumu letu ni kuhakikisha wawekezaji mnapata mazingira wezeshi katika fursa na miradi mnayotaka kuwezesha ili nchi iweze kupata tija kutokana uwekezaji huo” Amesisitiza Kairuki.
Akiongea katika kikao hicho mwenyekiti wa Bodi ya MNG Group of Companies, Mehmet Gunal, amefafanua kuwa , Kampuni hiyo iko tayari kuwekeza nchini katika Sekta ya Uchukuzi, Utalii, Nishati, Usafiri wa Anga na Ujenzi hapa nchini.
“Tumevutiwa na mazingira ya uwekezaji hapa nchini, Tanzania ndio maana nimeamua kampuni yetu iweze kujua fursa na miradi yenye kuhitaji uwekezaji nchini ili tuweze kukamilisha taratibu za uwekezaji na tuweze kuwekeza na tuko tayari kuwekeza hata kwa mfumo wa sera ya ushirikiano baina ya Sekta ya Binafsi na Umma au kuwekeza sisi wenyewe ” Masema Gunal
Kampuni ya MNG Group of Companies inao uzoefu katika masuala ya uwekezaji kwa miaka 42 katika mabara matatu Duniani, ikiwa imejikita katika uwekezaji kwenye sekta sita na tayari hadi hivi sasa imetekeleza miradi zaidi ya mia mbili katika mabara hayo.
Baadhi ya Miradi ambayo imetekelezwa na Kampuni hiyo ni pamoja na , Bwawa la kufua Umeme la Chief Dam la nchini Algeria, Ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa KOTOKA (terminal III), wa nchini Ghana, Ujenzi wa makao makuu ya Benki ya Halk nchini Uturuki, Uwanja wa mpira wa TIZI Ouzu pamoja na
Hivyo makala Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki Azungumza na Wawekezaji Kutoka Nchini Utruruki. Jijini Dodoma
yaani makala yote Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki Azungumza na Wawekezaji Kutoka Nchini Utruruki. Jijini Dodoma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki Azungumza na Wawekezaji Kutoka Nchini Utruruki. Jijini Dodoma mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/waziri-wa-nchi-ofisi-ya-waziri-mkuu.html
0 Response to "Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki Azungumza na Wawekezaji Kutoka Nchini Utruruki. Jijini Dodoma"
Post a Comment