Loading...

Arsenal matatani kufuzu robo fainali

Loading...
Arsenal matatani kufuzu robo fainali - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Arsenal matatani kufuzu robo fainali, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Arsenal matatani kufuzu robo fainali
link : Arsenal matatani kufuzu robo fainali

soma pia


Arsenal matatani kufuzu robo fainali

Arsenal wana kazi kubwa mikononi mwao kama wanataka kuendelea kuuota ubingwa wa Europa mwaka huu. Arsenal walipoteza mchezo kwa mabao 3-1 dhidi ya klabu ya kawaida kabisa kutoka ligi ya Ufaransa kwenye mechi ya kwanza ya mzunguko wa 16 bora wiki iliyopita na kwa sasa sasa wanahitaji walau magoli mawili bila majibu ili kufuzu kwenda hatua ya Robo fainali.

Vijana wa Unai Emery walipata ushindi muhimu dhidi ya Manchester United jumapili na morali yao imeongezeka maradufu, hata hivyo Arsenal watakuwa bila beki wao Sokratis ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita. Kocha huyo anatarajia kumuanzisha mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati dhidi ya Manchester United kwani anahitaji magoli zaidi ya kitu chochote ili aweze kufuzu.

Kwingineko Chelsea wako katika hali nzuri ukilinganisha na jirani zao wa jiji la London. Wao walifunga mabao 3-0 dhidi ya Dynamo Kyiv kwenye mchezo wa kwanza lakini walidondosha alama mbili siku ya jumapili walipokutana na Wolves kwenye ligi – matokeo ambayo yaliwafanya wasirejee katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi.

Kocha Maurizio Sarri anasema, “Ni kombe (Europa) la muhimu sana kwetu. Na kuna nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa kwa bingwa kwa hiyo lengo letu na ni muhimu kwetu kushinda.” Napoli ni timu nyingine iliyofanya vizuri wiki iliyopita baada ya kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Red Bull Salzburg, huku timu nyingine kutoka Serie A, Inter Milan ilitoka sare na Frankfurt walipokutana wiki iliyopita.

Ni StarTimes pekee ndio watakaokuonyesha ligi ya Europa kupitia chaneli zao za michezo. Arsenal vs Rennais saa 5:00 Usiku na utaonyeshwa LIVE kupitia ST World Football, Dynamo Kyiv vs Chelsea saa 2:55 Usiku nao pia utakuwa LIVE kupitia ST World Football.



Hivyo makala Arsenal matatani kufuzu robo fainali

yaani makala yote Arsenal matatani kufuzu robo fainali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Arsenal matatani kufuzu robo fainali mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/arsenal-matatani-kufuzu-robo-fainali.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Arsenal matatani kufuzu robo fainali"

Post a Comment

Loading...