Loading...
title : Balozi Seif Ali Iddi akutana na Waziri wa Kilimo na Rais wa Bunge la Cuba, ahudhuria maonesho ya kilimo nchini humo
link : Balozi Seif Ali Iddi akutana na Waziri wa Kilimo na Rais wa Bunge la Cuba, ahudhuria maonesho ya kilimo nchini humo
Balozi Seif Ali Iddi akutana na Waziri wa Kilimo na Rais wa Bunge la Cuba, ahudhuria maonesho ya kilimo nchini humo
Mkutano ukiendelea kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wa Cuba ukioongozwa na Mhe. Guastavo Rodriguez Roller. |
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ameipongeza Serikali ya Cuba kupitia Wizara ya Kilimo na Mifugo kwa mtazamo wake wa kuanzisha ushirikiano mpana zaidi baina ya Zanzibar na Tanzania katika sekta hiyo muhimu.
Akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Guastavo Rodriguez Roller, katika makao makuu ya wizara hiyo mjini Havana, Balozi Seif alieleza kuwa, Zanzibar na Cuba zimekuwa na ushirikiano ya karibu katika sekta za afya na elimu kwa kipindi kirefu sasa suala ambalo limeleta mafanikio makubwa.
Balozi Seif alibainisha kuwa, kwa kuwa maonyesho ni moja ya njia ya kubadilishana mawazo kitaaluma alimuomba Waziri wa Kilimo wa Cuba kutenga muda wa kushiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Tanzania yanayofanyika mwezi Agosti wa kila mwaka nchini.
Kwa upande wake, Mhe. Roller alibainisha kwamba, Cuba imebarikiwa kuwa na hekta milioni 10,000,000 ambazo zinatoa ajira kwa wakulima zaidi ya 5,000.Alifafanua kuwa, asilimia 70% ya ardhi hiyo ina maliasili, asilimia 3.5 inatumika kufuga na zaidi ya asilimia 60 inatumika katika uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na kilimo pekee.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Rais wa Bunge la Cuba, Mhe. Esteban Lazo Harnandez, mjini Havana, Cuba.
|
Mhe. Harnandez kulia akipokea zawadi ya mlango wa mji Mkongwe kutoka kwa Balozi Seif kama ishara ya kufunguliwa milango ya kuitembelea Zanzibar.
|
Mhe. Harnandez akimtembeza Mhe. Balozi Iddi katika sehemu mbalimbali za jengo la Bunge ya Cuba lenye historia ya muda mrefu ambazo zimewekwa kama kumbukumbu ya taifa hilo. |
Mhe. Balozi Iddi wa pili kutoka kulia na ujumbe wake akifanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Afya mjini Havana, Cuba.
|
============================== =======
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amelitembelea Bunge la Cuba na kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa bunge la nchi hiyo, Mhe. Esteban Lazo Harnandez.
Katika mazungumzo baina ya viongozi hao wawili, Mhe. Harnandez ameahidi kuwa, Cuba itaendelea kudumisha ushirikiano wake wa kidiplomasia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kuendeleza wananchi wake licha ya taifa hilo la Caribean kupita katika mabadiliko ya kisiasa, uchumi na utamaduni.
Mhe. Harnandez alieleza kuwa, kutokana na mabadiliko yaliyopo sasa katika mfumo wa dunia katika masuala ya uchumi, siasa na utamaduni Jamhuri ya Cuba imelazimika kufanya mabadiliko ya katiba yake ili yalingane na mfumo huo wa dunia inayoizunguka.
Alifafanua kuwa, tayari Bunge la Cuba limeshafanya marekebisho katika katiba yake kutoa nafasi kwa wananchi wake kuwa na uwezo na uhuru wa kumiliki nyumba, ardhi pamoja na uwepo wa waziri mkuu atakayekuwa na mamlaka ya kusimamia utendaji wa serikali.
Mhe. Harnandez alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, kwamba katika vikao vya bunge hilo vinavyotarajiwa kuanza wiki ijayo baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa wabunge, serikali ya nchi hiyo itakuwa imepiga hatua kubwa zaidi ya maendeleo kutokana na mabadiliko hayo.
Rais huyo wa Bunge la Cuba alisisitiza kwamba taasisi za kifedha zitalazimika kuzingatia ukusanyaji bora zaidi wa mapato katika maeneo yote ya uchumi ili kuimarisha ushiriki wa wananchi waliowengi katika mfumo huo.
Mhe. Harnandez alihitimisha kwa kumuhakikishia Balozi Seif kwamba, uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya pande hizo mbili utaendelea kuimarishwa na kukuzwa katika muda wote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Iddi alimpongeza Mhe. Harnandez kwa kuchaguliwa tena kuliongoza bunge hilo na kueleza kuwa, hatua hiyo inaonesha wazi ishara halisi ya kukubalika vyema na wananchi wa nchi hiyo kupitia viongozi wake.
Halikadhalika, Mhe. Balozi Iddi alieleza kuwa, kwa ujumla Zanzibar itaendelea kufuatilia mabadiliko ya Cuba na kuangalia endapo inaweza kuiga mabadiliko hayo ili kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi walio wengi.
Mhe. Balozi Iddi na ujumbe wake ulihitimisha ziara yake nchini humo kwa kufanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Afya ya Cuba uliokuwa ukiongozwa na Naibu Waziri, Mhe. Bibi Marcia Cobas, katika makao makuu ya wizara hiyo yaliyopo Havana, Cuba.
Katika mazungumzo hayo ya ushirikiano wa kindugu, Balozi Iddi alisema matunda ya darasa la madaktari wazalendo waliosimamiwa na wataalamu pamoja na wahadhiri wa nchi ya Cuba yameanza kutoa matumaini.Alifafanua kuwa, kitendo cha Serikali ya Cuba kukubali kupunguza gharama kubwa ya kuwaendeleza madaktari hao wazalendo wapatao 15 katika shahada ya juu ya udaktari wa uzamili nchini humo kinaendelea kuleta faraja kubwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na watu wake.
Alisema wakati Zanzibar ikiendelea kutekeleza sera ya afya ya kuwa na miuondombinu ya huduma za afya katika umbali usiozidi kilomita tano kundi hilo na madaktari linaloendelea kuongezeka kila mwaka litakuwa mkombozi wa utekelezaji wa sera hiyo muhimu.
Naye Kaibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Bibi Asha Ali Abdullah, aliueleza uongozi huo wa Wizara ya Afya Cuba kwamba, hivi sasa Zanzibar inapita katika kipindi cha kujiimarisha kwenye mapambano yake dhidi ya maradhi yasiyoambukiza.
Bibi Abdullah alisema maradhi yasiyoambukiza kama Kisukari pamoja na Shindikizo la Damu hivi sasa yamekuwa yakiathiri wananchi walio wengi na kuleta vifo vingi. Hata hivyo, jitihada zinachukuliwa ili kupunguza kasi ya athari za maradhi hayo na kuimaliza kabisa kadhia hiyo kabisa.
Alibainisha kuwa, maradhi ya Malaria hivi sasa yamepungua kutokana na kampeni kubwa iliyofanywa na serikali kwa kushirikiana na taasisi na mataifa wahisani katika kuangamiza vilui lui vya maradhi hayo.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya Zanzibar alimuhakikishia Naibu Waziri wa Afya wa Cuba kwamba ushauri wote walioupata katika ziara yao kwenye taasisi za Afya nchini Cuba likiwemo suala la upatikanaji wa dawa litazingatiwa na iwapo linaweza kuleta afueni ya gharama kwa Zanzibar litachukuliwa hatua mara moja.
Hivyo makala Balozi Seif Ali Iddi akutana na Waziri wa Kilimo na Rais wa Bunge la Cuba, ahudhuria maonesho ya kilimo nchini humo
yaani makala yote Balozi Seif Ali Iddi akutana na Waziri wa Kilimo na Rais wa Bunge la Cuba, ahudhuria maonesho ya kilimo nchini humo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Seif Ali Iddi akutana na Waziri wa Kilimo na Rais wa Bunge la Cuba, ahudhuria maonesho ya kilimo nchini humo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/balozi-seif-ali-iddi-akutana-na-waziri.html
0 Response to "Balozi Seif Ali Iddi akutana na Waziri wa Kilimo na Rais wa Bunge la Cuba, ahudhuria maonesho ya kilimo nchini humo"
Post a Comment