Loading...
title : Baraza la Wazee Asilia watoa msaada kwa Wagonjwa Mloganzila
link : Baraza la Wazee Asilia watoa msaada kwa Wagonjwa Mloganzila
Baraza la Wazee Asilia watoa msaada kwa Wagonjwa Mloganzila
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Redemptha Matindi akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada wa sabuni, mafuta ya kujipaka uliotolewa leo hospitalini hapo.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Sista Redemptha Matindi akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Baraza hilo leo katika Hospitali ya Mloganzila.
Kiongozi wa wodi ya wagonjwa wa magonjwa ya ndani Muuguzi Lucas Mwaijega (kulia) akikabidhiwa msaada na Katibu wa baraza hilo Mzee. Ahmad Tamla.
Baraza la Wazee Asilia Mbezi Luis Jijini Dar es salaam (BAWAZI) leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na kutoa msaada wa mafuta, sabuni pamoja na pampers kwa baadhi ya wagonjwa ambao hawajiwezi.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Mloganzila Redemptha Matindi amewashukuru wazee hao kwa kujitoa na kuamua kuwasaidia baadhi ya wagonjwa ambao wanaendelea na matibabu hospitalini hapo na hawana uwezo wa kununua mahitaji yao mbalimbali.
“Tumefurahi kupokea msaada huu ambao kimsingi umewalenga wale wasiojiweza ni faraja kwetu kuona wazee kama nyinyi mkijitoa kwa ajili ya jamii hakika huu ni mfano wa kuigwa na watu wote’’. Amesema Sista Redemptha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza hilo Mzee Abdallah Shomari amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.
“Tumeguswa na hali ya wagonjwa wasiojiweza na ndio maana tumeamua kuja kuwapatia tulichonacho, lakini pia hospitali hii ipo katika Manispaa yetu ya Ubungo hivyo tumeona ni muhimu kuja kuwatembelea wagonjwa hawa na kuwapatia msaada wa mafuta ya kujipaka, sabuni na pampers, tutaendelea kujitoa kadiri uwezo utakavyoruhusu’’. Amesema Mzee Shomari.
Pamoja na mambo mengine wazee hao pia wameelezea kuridhishwa na utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Mloganzila na kutoa wito kwa jamii kuthamani na kutambua huduma zinazotolea hospitali hapo kwani ni za uhakika na zenye ubora wa juu.
Hivyo makala Baraza la Wazee Asilia watoa msaada kwa Wagonjwa Mloganzila
yaani makala yote Baraza la Wazee Asilia watoa msaada kwa Wagonjwa Mloganzila Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Baraza la Wazee Asilia watoa msaada kwa Wagonjwa Mloganzila mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/baraza-la-wazee-asilia-watoa-msaada-kwa.html
0 Response to "Baraza la Wazee Asilia watoa msaada kwa Wagonjwa Mloganzila"
Post a Comment