Loading...
title : Waziri Mkuu atembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) jijini Dar es salaam
link : Waziri Mkuu atembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu atembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) jijini Dar es salaam
Na WAMJW - Dar Es Salaam
Serikali imedhamiria kushughulikia malalamiko yaliyotolewa na wafanyabiashara kuhusu mkanganyiko wa majukumu baina ya Taasisi za Serikali zinazoingiliana majukumu na kuzitaka kila taasisi kama hizo ziwe na mipaka yake ya kazi na kupunguza urasimu.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza na watendaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA mapema leo alipotembelea ofisi hizo kujionea utendaji wao wa kazi.
Waziri Majaliwa amesema Taasisi za Serikali ambazo zimekuwa zikiingiliana majukumu na zimekuwa zikisababisha adha kwa wananchi na kuongeza urasimu na upotevu wa muda mwingi katika kuwahudumia wateja.
“Serikali imedhamiria kutafuta ufumbuzi wa malalamiko ya mwingiliano wa majukumu baina ya taasisi za Serikali ili kumwondolea usumbufu mwananchi” amesema Waziri Majaliwa na kuendelea kusema kuwa mkanganyiko huo unapelekea watu kutokujua majukumu yao aidha kwa kutokujua sheria au kwa makusudi.
Waziri Majaliwa amesema kumekuwa na malalamiko mengi ya utendaji usiyo sahihi wa mwingiliano wa majukumu hasa kwenye eneo la ukaguzi na uchukaji wa sampuli baina ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na kuzitaka taasisi hizo kujiridhisha na kuyafahamu vizuri majukumu yao.
Kufuatia hali hiyo Waziri Kassim Majaliwa amewataka Viongozi wa Wizara ya Afya, Wizara ya Kilimo, Mifugo,Wizara ya Viwanda na Uwekezaji kuwasilisha ofisini kwake ripoti ya utekelezaji wa “Blueprint” ifikapo Machi 30 mwaka huu.
Aidha, Waziri Majaliwa ameitaka TFDA kujiimarisha zaidi kwenye ukaguzi wa vyakula na dawa na kuhakikisha bidhaa zisizokuwa na usajili haziingii sokoni na kuitaka TFDA kuongeza wataalam katika Mikoa na Wilaya ili kudhibiti mapito ya magendo ya bidhaa za chakula na dawa.
Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Serikali imewekeza fedha nyingi katika maabara za uchunguzi wa vyakula na dawa na hivi sasa taasisi hiyo imefikia ngazi ya tatu ya ubora wa udhibiti wa dawa kimataifa hivyo kuaminika na mataaifa mbalimbali na kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi kuja kuingiza bidhaa zao nchini.
Waziri Ummy amesema kuwa TFDA imepewa dhamana ya kulinda afya za watanzania kwa kuhakikisha vyakula na dawa zinazozitumia kila siku ni salama kwa afya za wananchi na kukiri kuwa kweli changamoto zipo na kupitia wizara yake atahakikisha changamoto hizo zinatatuliwa ndani ya muda mfupi.
Naye ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angellah Kairuki amesema kuwa Serikali imeanzisha huduma ya mahali pamoja iliyopo katika kituo cha uwekezaji (TIC) ambapo mpaka sasa zipo taasisi 16 ikiwemo TFDA huku akiomba Wizara husika kuongeza watumishi katika kitengo hicho ili kuweza kushughulikia kwa uharaka masuala ya uwekezaji katika vyakula na dawa.
Aidha,Waziri Kairuki amekiri kuwepo mkakanganyiko wa majukumu baina ya taasisi za Serikali huku akiitaka TFDA kutowahudumia wawekezaji wanaofika nchini wakiwa na Vyeti vya Usajili wa Vivutio kwani wanatakiwa kuhudumiwa na TIC.
"Naomba kuweka msisitizo, mara anapokuja mwekezaji, swali lenu la kwanza liwe ni kuuliza kama anacho Cheti cha usajili wa vivutio kutoka TIC au la, na endapo anayo basi nyinyi mwelekezeni TIC".Alisisitiza Waziri Kairuki
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akisema jambo na watendaji wa ofisi ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) hawapo pichani alipotembelea ofisi hizo kuona utendaji kazi wao.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wa (wa tatu kutoka kushoto) akiongozana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaj Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) kuelekea maabara za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika dawa ya malaria aina ya DUO -COTECXIN, halisi kulia na bandia kushoto zilizopimwa na Maabara ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakati alipotembelea ofisi za TFDA, wa pili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki na wa tatu kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akionyeshwa sampuli na Dkt. Yonah Hebron Meneja wa Uchunguzi wa Dawa na Bidhaa katika maabara ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mapema leo alipotembelea ofisi hizo kujionea utendaji kazi wao.
Hivyo makala Waziri Mkuu atembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) jijini Dar es salaam
yaani makala yote Waziri Mkuu atembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) jijini Dar es salaam Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mkuu atembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) jijini Dar es salaam mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/waziri-mkuu-atembelea-mamlaka-ya.html
0 Response to "Waziri Mkuu atembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) jijini Dar es salaam"
Post a Comment