Loading...
title : Benki ya Exim yazidi kujiimarisha, yainunua benki ya UBTL
link : Benki ya Exim yazidi kujiimarisha, yainunua benki ya UBTL
Benki ya Exim yazidi kujiimarisha, yainunua benki ya UBTL
Benki ya Exim Tanzania imezidi kujitanua na kujiimalisha zaidi hapa nchini baada ya kuonesha nia na utayari wa kuinunua rasmi kuwa benki ya UBL Tanzania Limited (UBTL) kwa asilimia 100. Hii ikiwa ni baada ya kusainishana barua ya kuonesha nia (Letter of Intent)
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Bw Jaffari Matundu, inasema ununuzi huo unaohusisha mali na madeni unazidi kuifanya benki hiyo ambayo kwasasa ni miongoni mwa benki tano kwa ukubwa hapa nchini kuzidi kujitanua zaidi ndani na nje ya nchi.
“Kwetu ni furaha kubwa kuona kwamba familia yetu inazidi kuongezeka kwa kuwa tayari tunaungana na wanafamilia kutoka benki ya UBTL . Zaidi ya yote tunaamini pia kuwa wafanyakazi wa benki ya UBTL wataongeza nguvu ambayo kwa pamoja tutaweza kutoa huduma bora zaidi za kibenki kwa wateja wa UBTL,’’ alisema bw Matundu.
Alisema kuwa benki ya Exim inatarajia kukaribisha wateja wa benki ya UBTL katika mtandao mpana wa matawi ya benki ya Exim huku akiongeza kuwa hatua ya ununuzi huo ni upanuzi wa asili na uimarishaji wa uwepo wa benki hiyo katika soko la ndani ya nchi.
Benki ya Exim ilianzishwa mwaka 1997 na ndio benki ya kwanza hapa nchini kuvuka mipaka na kujiimarisha nje ya nchi ambapo kwasasa imefanikiwa kuwa na matawi yake katika nchi za Uganda, Comoro and Djibouti.
Tangu kuanzishwa kwake benki hiyo imekuwa ikijipambanua kwa ubora wa huduma ikilenga kujenga thamani ya uwekezaji kwa wadau wake na kufikia ukuaji wake kwa kutoa huduma kwa upekee na iliyoboreshwa.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa UBTL Bw Gasper Njuu alisema benki hiyo pamoja na wanahisa wake wamekuwa na mtazamo chanya juu ya fursa za ukuaji nchini Tanzania na kwasasa hilo linakwenda kufanikiwa kupitia benki ya Exim.
“Wakati tukiwa kwenye mkakati wa mabadiliko ya kibiashara kupitia uwekezaji zaidi kwenye huduma za kidigitali ndipo tulipokea ombi kutoka benki ya Exim wakiomba kununua benki ya UBTL na baada ya kufikiria kwa kina pande zote wakiwemo wanahisa wetu walikubaliana na ombi hilo hasa kwa kuzingatia ubora, weledi na sifa za benki ya Exim kwa hapa nchini ambao kimsingi unaleta tija kubwa kwa wadau na wateja wetu,’’ alibainisha bw Njuu
Benki ya UBTL ilianzishwa mwaka 2013, kama benki tanzu inayomilikiwa na Benki ya United Bank Limited (UBL) ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini Pakistan na imetoa huduma za benki za rejareja na za jumla kwa wateja mbalimbali.
Alisema hatua ya ununuzi inahusisha taratibu kadhaa za kisheria zikihusisha nchi za Tanzania na Pakistan na zinatarajiwa kukamilika katikati ya mwaka 2019.
Kufuatia hatua hiyo pande zote yaani Benki ya Exim na UBTL wameahidi kushirikiana vyema na Benki Kuu ya Tanzania ndani ya wiki zijazo kuhakikisha kwamba mabadiliko hayo yanafanyika kwa urahisi na kwa kuzingatia taratibu zote za kisheria.
Hivyo makala Benki ya Exim yazidi kujiimarisha, yainunua benki ya UBTL
yaani makala yote Benki ya Exim yazidi kujiimarisha, yainunua benki ya UBTL Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya Exim yazidi kujiimarisha, yainunua benki ya UBTL mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/benki-ya-exim-yazidi-kujiimarisha.html
0 Response to "Benki ya Exim yazidi kujiimarisha, yainunua benki ya UBTL"
Post a Comment