Loading...
title : Benki ya UBA yazindua shughuli Uingereza.
link : Benki ya UBA yazindua shughuli Uingereza.
Benki ya UBA yazindua shughuli Uingereza.
LONDON, UINGEREZA
WIKI tatu tu baada ya Kundi la Himaya ya Kibenki la United Bank of Africa (UBA Group) kuzindua shughuli zake nchini Mali, limefanya hivyo pia katika jiji la London, Uingereza.
Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa hafla maalumu Alhamisi iliyopita wakati jiji hili la kibiashara lilipokuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa kibiashara na sekta ya umma.
Katika hafla maalumu ya mkutano huo, UBA UK ilitambulishwa rasmi kwa viongozi wa kibiashara kutoka Ulaya na Afrika ikiwa na dhamira na utayari wa kuchochea biashara baina ya mabara hayo.
Kwa uzinduzi huo, UBA Group inazidi kujipanua katika sekta ya kibenki ikiwa kama taasisi ya kwanza na pekee ya kifedha kusini mwa jangwa la Sahara Afrika inayoendesha shughuli nchini Uingereza na Marekani.
Hilo linaifanya kuzidi kuitambulisha hadhi yake kama benki ya kidunia kutoka Afrika inayowezesha biashara na mtiririko wa mitaji baina ya Afrika na Dunia.
Akizungumza katika tukio hilo, Mwenyekiti wa UBA Group, Tony Elumelu alisema benki imefurahishwa na mamlaka za Uingereza kuiruhusu kuimarisha na kupanua operesheni zake na hivyo kutimiza dhamira yake ya kupanua biashara na uwekezaji baina ya Afrika na Ulaya.
Elumelu pia alieleza furaha yake kuona UBA kama benki kutoka Afrika inavyoweza kuchomoza na kusaidia wawekezaji katika miji muhimu ya kifedha duniani.
Akizungumza katika tukio hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa UBA Group, Kennedy Uzoka, alisema; “Wakati huo huo tunahudumia mahitaji ya kibiashara na mitaji kwa wateja wetu wa Afrika, ambao wanatafuta masoko Ulaya.
“Kwa kuzindua UBA UK Limited, tunafurahi kupanua huduma hizo kwa wateja wa sasa, wakati huo huo tukikaribisha wapya waweze kikamilifu kutimiza ndoto zao za kifedha kupitia mtandao wetu wa kibenki.”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Uingereza, Patrick Gutmann, Mkurugenzi Mtendaji, UBA Plc, Kennedy Uzoka, Rais Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote, Mwenyekiti wa UBA Group, Tony Elumelu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wakati wa uzinduzi wa UBA London nchini Uingereza.
Hivyo makala Benki ya UBA yazindua shughuli Uingereza.
yaani makala yote Benki ya UBA yazindua shughuli Uingereza. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya UBA yazindua shughuli Uingereza. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/benki-ya-uba-yazindua-shughuli-uingereza.html
0 Response to "Benki ya UBA yazindua shughuli Uingereza."
Post a Comment