Loading...

Serikali yawekeza nguvu miradi ya maji -Profesa Mbarawa

Loading...
Serikali yawekeza nguvu miradi ya maji -Profesa Mbarawa - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Serikali yawekeza nguvu miradi ya maji -Profesa Mbarawa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Serikali yawekeza nguvu miradi ya maji -Profesa Mbarawa
link : Serikali yawekeza nguvu miradi ya maji -Profesa Mbarawa

soma pia


Serikali yawekeza nguvu miradi ya maji -Profesa Mbarawa

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

SERIKALI imesema kuwa hali ya upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 66 hivyo nguvu zaidi inatumika katika kuhakikisha inafikia asilimia 90 wakati mkoa wa Dar es Salaam ukiwa na asilimia 85 ya upatikanaji wa maji.

Hayo ameyasema Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakati akitangaza maadhimisho ya wiki ya maji ambayo hufanyika Machi 22 ya kila mwaka,amesema kuwa serikali imewekeza katika miradi ya maji katika kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Profesa Mbarawa amesema azimio la Umoja wa Mataifa ulizitaka nchi wanachama kuanzia mwaka 1993 kutenga siku hii kuwa siku maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma kuhusu sekta ya maji kwa njia mbalimbali, kama vile machapisho, mikutano, semina na maonesho. Lengo la maadhimisho haya ni kukuza uelewa kwa umma kuhusu umuhimu wa maji katika shughuli za uchumi, kijamii na maisha kwa ujumla.

Amesema maadhimisho hayo yamekuwa yakiadhimishwa siku ya maji duniani kwa kuandaa shughuli mbalimbali zinazochochea ushiriki wa umma katika kulinda na kuendeleza rasilimali za maji na Shughuli mbalimbali zikiwemo kwa njia ya mikutano, semina, warsha na maonesho. 

Mbarawa amesema maadhimisho ya siku ya maji yataanza Machi 16 na kuhitimishwa Machi 22 kwa Shughuli mbalimbali zikiwemo mikutano, warsha, semina, maonesho, pamoja na ukaguzi na uzinduzi wa miradi ya maji. 

Amesema katika siku ya maadhimisho ya wiki ya maji kutambua umuhimu wa kufikia malengo yaliyowekwa ya kupanua huduma ya maji ifikapo mwaka 2020, kauli mbiu ya siku ya maji ya mwaka 2019 imepangwa kuwa: “Hakuna Atakayeachwa: Kuongeza Kasi ya Upatikanaji wa Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa Wote katika dunia inayobadilika kitabia nchi. 

Aidha amesema pamoja na shughuli mbalimbali zitakazofanyika nchi nzima, ikiwemo ukaguzi na uzinduzi wa Mkutano wa kitaifa wa mwaka wa maji utakaoshirikisha wadau na wataalamu wa maji utakaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya St. Gaspar Jijini Dodoma.

Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Mafuta EWURA itazindua na kuwasilisha Ripoti ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini ya mwaka 2017/18; na kuwashirikisha wadau kuhusu shughuli za udhibiti katika Sekta ya Maji .

Katika kilele cha maadhimisho hayo kutakuw na Mkutano wa Mapitio ya Sekta ya Maji ni maalumu kwa wadau kutathmini utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) nchini.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Wiki ya Maji itakyofanyika kuanzia Machi 16 hadi 22.


Hivyo makala Serikali yawekeza nguvu miradi ya maji -Profesa Mbarawa

yaani makala yote Serikali yawekeza nguvu miradi ya maji -Profesa Mbarawa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Serikali yawekeza nguvu miradi ya maji -Profesa Mbarawa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/serikali-yawekeza-nguvu-miradi-ya-maji.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Serikali yawekeza nguvu miradi ya maji -Profesa Mbarawa"

Post a Comment

Loading...