Loading...

COCA COLA KWANZA YAZINDUA KAMPENI YA ‘MWANAMKE SHUJAA’ KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Loading...
COCA COLA KWANZA YAZINDUA KAMPENI YA ‘MWANAMKE SHUJAA’ KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa COCA COLA KWANZA YAZINDUA KAMPENI YA ‘MWANAMKE SHUJAA’ KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : COCA COLA KWANZA YAZINDUA KAMPENI YA ‘MWANAMKE SHUJAA’ KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
link : COCA COLA KWANZA YAZINDUA KAMPENI YA ‘MWANAMKE SHUJAA’ KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

soma pia


COCA COLA KWANZA YAZINDUA KAMPENI YA ‘MWANAMKE SHUJAA’ KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI



Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa akizungumza na wafanyakazi wa kike wa kampuni hiyo walioungana na ‘Mama Lishe’ wa Soko la Tandale wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.
Mwakilishi wa akina mama wanaofanya biashara ya chakula maarufu kama ‘Mama Lishe’ katika Soko la Tandale, Stamil Gereza (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa kike wa kampuni ya Coca Cola Kwanza walioungana na ‘Mama Lishe’ wa Soko la Tandale wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa (katikati) na Meneja Rasilimali watu wa Kampuni hiyo Naomi John (kulia).
Sehemu ya wafanyakazi wanawake wa Coca Cola Kwanza waliojiunga na akina ‘Mama Lishe’ kutoka Tandale wakipanga mstari kupata chakula wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.


Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa akitoa huduma kwa wafanyakazi wanawake wa Coca Cola Kwanza ambao waliungana na ‘Mama Lishe’ wa soko la Tandale wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.
Mratibu na mtaalamu wa masuala ya Vicoba kwa akina mama, Anitha Ngoya akikata keki kwa niaba ya akina Mama Lishe wa Soko la Tandale ambao waliungana na wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Coca Cola Kwanza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.
Mtaalamu wa utambuzi wa Soko kutoka Kampuni ya Coca Cola Kwanza, Jacqueline Rimoy akiwasaidia akina Mama Lishe wa soko la Tandale kupika wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.

Sehemu ya wafanyakazi wanawake wa Coca Cola Kwanza waliojiunga na akina ‘Mama Lishe’ kutoka Tandale wakipanga mstari kupata chakula wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.



Coca-Cola Kwanza imezindua kampeni ya kusherehekea mafanikio ya wanawake ya “Mwanamke Shujaa” ili kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake mwaka huu.

Kampeni hiyo imelenga kubadilisha dhana ya kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu, kulingana na maudhui ya mwaka huu.

Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea Uwezeshaji wa Kijinsia.

Kampeni hii imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao.

Leo, wafanyakazi wa kike katika kampuni yetu wamejumuika pamoja na akina ‘Mama Lishe’

wa Soko la Tandale katika kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Coca- Cola Kwanza, Josephine Msalilwa alisema kuwa, lengo lao ni kusherehekea na kuhamasisha wanawake kutoka sekta tofauti na pia kuwaonyesha kwamba wanathaminiwa.

“Ni kuhusu kusherehekea mafanikio ya wanawake na kuwahamasisha kwamba pia wanaweza kufikia malengo yao na kufikia mafanikio makubwa,”amesema Msalilwa.

Msalilwa aliongeza kuwa, kampuni yao inao wajibu katika jamii, hivyo wanaamini kuwa ni wajibu wao kuleta mabadiliko endelevu katika sekta mbalimbali ambazo wanawake wa Tanzania wanafanya kazi zao, hivyo kuanzishwa kwa kampeni hiyo ni hatua muhimu.

“Nimekutana na wanawake wengi waliofanya mambo makubwa nchini Tanzania, ambao wameamua kuvunja vikwazo na kufikia mafanikio makubwa,”aliongeza.

Pia akizungumza wakati wa tukio hilo, Stamil Gereza mwakilishi wa akina Mama Lishe kutoka Tandale alimuelezea mwanamke kama mtu mwenye akili na uwezo wa kujitegemea.

Aliwahimiza wanawake kuanza kusimama kidete na kufanya mambo yote wanayoamini katika jamii licha ya changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo.

Kwa upande wake, Anitha Ngoya Mratibu na mtaalamu wa masuala ya Vicoba kwa akina mama ambaye amekuwa akiwafundisha akina Mama Lishe juu ya ujasiriamali, usimamizi wa kifedha kwa niaba ya Coca Cola Kwanza alisema, "Mpaka sasa tumewafundisha wanawake zaidi ya 45 kwenye mtandao wetu wa akina mama wajasiriamali na bado tunajitanua zaidi ". Lengo letu ni kuwafikia wanawake zaidi ya 300 kila mwaka.

Coca-Cola Kwanza imekuwa ikijihusisha katika mipango mbalimbali endelevu ambayo inalenga kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake nchini Tanzania.

Ikiwemo kampeni ya ufukweni ya “Mchanga Pekee” ambayo ilizinduliwa hivi karibuni ambapo wanawake wengi wameajiriwa kwa ajili ya kufanya usafi, kukusanya chupa za plastiki katika fukwe mbalimbali nchini.

Kupitia Kampeni ya 5by20, ambao ni mpango wa Coca-Cola wa Kimataifa kutoa usaidizi wa kiuchumi kwa wanawake milioni 5 kwa ajili ya kuendesha biashara zao katika nchi zote duniani ifikapo 2020, Coca-Cola Kwanza imesaidia kujenga vibanda vinavyotumiwa na Mama Lishe ambao wapo nje ya kiwanda hicho. Pia Coca-Cola Kwanza imewawezesha wanawake hao kwa kuwapatia mitungi ya gesi ya kilo 15.


Hivyo makala COCA COLA KWANZA YAZINDUA KAMPENI YA ‘MWANAMKE SHUJAA’ KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

yaani makala yote COCA COLA KWANZA YAZINDUA KAMPENI YA ‘MWANAMKE SHUJAA’ KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala COCA COLA KWANZA YAZINDUA KAMPENI YA ‘MWANAMKE SHUJAA’ KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/coca-cola-kwanza-yazindua-kampeni-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "COCA COLA KWANZA YAZINDUA KAMPENI YA ‘MWANAMKE SHUJAA’ KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI"

Post a Comment

Loading...