Loading...
title : DAWASA YATATUA ASILIAMIA 70 YA MALALAMIKO KATIKA WIKI YA JAMII
link : DAWASA YATATUA ASILIAMIA 70 YA MALALAMIKO KATIKA WIKI YA JAMII
DAWASA YATATUA ASILIAMIA 70 YA MALALAMIKO KATIKA WIKI YA JAMII
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam imetatua asilimia 70 ya malalamiko yaliyotolewa na wananchi kwenye maadhimisho ya wiki ya maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Maadhimisho ya wiki ya maji yalifanyika kuanzia Machi 16-22 mwaka huu kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA Bi Neli Msuya amesema kuwa jumla ya wakazi zaidi ya 400 waliweza kufika kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja na kutoa maoni na malalamiko mbalimbali yaliyolenga kuboresha huduma za DAWASA.
Amesema, kwenye maadhimisho ya mwaka huu waliweza kufungua dawati maalum la kupokea taarifa, kero, malalamiko na maoni ya wananchi juu ya huduma zinazotolewa na DAWASA na kwa asilimia kubwa hilo limefanikiwa.
Msuya amesema, kwenye dawati maalum kulikuwa na wataalamu wa DAWASA wa fani mbalimbali na kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwasikiliza wananchi waliojitokeza kwenye Maadhimisho hayo.
"Kwanza napenda kuwashukuru wateja wote na wananchi kwa ujumla waliojitokeza kuungana na Mamlaka katika maadhimisho ya wiki ya maji yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa Mkoa wa Dar es Salaam na wameweza kutoa kero, maoni na ushauri mbalimbali ambapo asilimia 70 ya malalamiko tumeshafanyia kazi na zingine zipo kwenye hatua ya ufuatiliaji kwenye idara husika," amesema Msuya.
Ameeleza kuwa, DAWASA wamedhamiria kuboresha utaratibu wa kupokea maoni kwa wateja ikiwa ni pamoja na kuwa na dawati linalohama kutoka eneo moja hadi lingine litakalojulikana kama 'mobile customer care desk' ili kufikia wakazi wengi na kupokea maoni mengi zaidi kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi wanaohudumiwa na DAWASA.

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso alipotembelea maonyesho ya Mamlaka ya Majisafi na majitaka DAWASA akiwa pamoja na wananchi waliofika kwa ajili ya kupata maelezo mbalimbali kuhusiana na Mamlaka hiyo kwenye dawati la Afisa wa DAWASA.
Hivyo makala DAWASA YATATUA ASILIAMIA 70 YA MALALAMIKO KATIKA WIKI YA JAMII
yaani makala yote DAWASA YATATUA ASILIAMIA 70 YA MALALAMIKO KATIKA WIKI YA JAMII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DAWASA YATATUA ASILIAMIA 70 YA MALALAMIKO KATIKA WIKI YA JAMII mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/dawasa-yatatua-asiliamia-70-ya.html
0 Response to "DAWASA YATATUA ASILIAMIA 70 YA MALALAMIKO KATIKA WIKI YA JAMII"
Post a Comment