Loading...

KWA TANESCO HII MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU...

Loading...
KWA TANESCO HII MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU... - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KWA TANESCO HII MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU..., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KWA TANESCO HII MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU...
link : KWA TANESCO HII MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU...

soma pia


KWA TANESCO HII MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU...



Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MACHO yangu yanashuhudia kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Shirika la Umeme  Tanzania(TANESCO) chini ya Wizara ya Nishati kwa niaba ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.

Kubwa zaidi masikio yangu kwa miaka miwili sasa yamekuwa yakisikia sifa zikitolewa kwa TANESCO kwasababu tu yale mambo ya kukatika katika kwa umeme yamepungua .Tulizoea kuita mgao.Mara umeme unatika...mara huooooo umerudi.Leo hii umeme ukikatika basi ni kwasababu maalumu na umma utakuwa umeshapata taarifa mapema.Mbona raha jamani.

Kwangu mimi najaribu kuiangalia TANESCO ya sasa na ile ya zamani.Kuna tofauti kubwa ya kiutendaji.TANESCO ya sasa chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Dk. Tito Mwinuka inajua umuhimu wa nishati ya umeme.Inajua kabisa uchumi wetu unahitaji uwepo wa umeme wa uhakika katika kufanya shughuli zao za kila siku.

TANESCO inayoongozwa na Dk.Mwinuka inajua umuhimu wa kutoa taarifa kwa wananchi hasa pale ambapo kutakuwa na matenengezo katika eneo fulani.TANESCO ya sasa inajua kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inataka kuelekea uchumi wa kati ambao utachagwiza na umeme wa uhakika.

Pia inatambua fika kama kuna eneo ambalo lilikuwa linalalamikiwa ni kukatika kwa umeme.Mgao wa umeme ulikuwa kero kwa watu wengi.Tena kero haswaa na najua sio kwangu tu hata kwako.Ndio mgao ilikuwa kero.Unabisha?

Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutambua nchi yoyote ili iendelee inahitahaji kuwa na nishati ya umeme wa kutosha na uhakika.Ndio maana leo hii TANESCO inaendelea na ujenzi wa miradi mikubwa na midogo ya umeme ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake.

Kutekelezwa kwa miradi hiyo na hasa kwenye maeneo ambayo awali yalikuwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara leo hii hakuna tena mgao.Wananchi wanafurahia nishati hiyo ya umeme wa uhakika.Ukitaka kuamini hili inaloeleza hapa nenda mikoa ya Kaskazini ikiwemo ya Arusha na Kilimanjaro.Hawana tena tatizo la kukatika kwa umeme kama zamani.

Sote tunafahamu kabla ya Awamu ya Tano kuingia madarakani kulikuwa na changamoto kubwa ya umeme.Leo hii imebaki historia.Umeme unaozalishwa Mkoa wa Arusha umekidhi mahitaji na kufanya kuwepo na umeme wa akiba.Hivyo ninaposema TANESCO inastahili pongezi sio kwamba natoa sifa sehemu ambayo haistahili.

Hongereni TANESCO kazi ambayo mnaifanya kwa niaba ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kubwa na tunaiona. Pamoja na mambo mengine , TANESCO kwa sasa wanaendelea na majukumu ya kuendelea kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya nishati ya umeme.

Na si tu kuondoa changamoto,pia imeendelea na wajibu wake mkubwa kusambaza umeme kwa wananchi.Nafahamu jitihada za kupeleka umeme kwa kila kijiji ndani ya nchi yetu kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Naomba niwe mkweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.Hakika Wizara ya Nishati na TANECSO wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha umeme unafika kwa kila Mtanzania anayeuhitaji.Kwa siku mbili hizi nimekuwa nikishuhudia baadhi ya nyumba tena za matembe zikiwa zimewekwa umeme.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia tu, umeme unawekwa vijijini ila kwa bahati mbaya tupo baadhi yetu ni kama Tomaso.Bila kuona hakuna kuamini.Sasa tunaamini kumbe kweli.Hivyo uwepo wa picha hizo ambazo zinaonesha nyumba za udongo zikiwa zimewekwa umeme inaleta maana halisi ya kile ambacho Wizara ya Nishati inafanya kwa wananchi wake.

Tunafahamu kauli mbiu ya TANESCO imekuwa ikisema "Tunaangaza maisha" .Nimeamini hata uwe kijijini bado utaangaziwa maisha.Hili ni jambo jema na la kupongezwa.Umeme wa uhakika vijijini ni jambo la msingi sana, na tunafahamu kwa muda mrefu vijiji vyetu vilikosa maendeleo kwasababu ya kutokuwa na umeme.Leo wanao.

Kwa waliobahatika kuishi maeneo ya vijijini wanafahamu mazingira ya kutokuwa na umeme.Wana vijiji wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta nishati ya umeme.Ameaniaka mahindi au mpunga wake lakini linapofika suala la kusaga au kukoboa anawaza umbali wa kwenda mashineni.Leo hii hakutakuwa na kuwaza tena.

Umeme unapatikana kila mahali.Shida iko wapi? Hata hivyo, kuna baadhi ya watu kwenye mitandao nimeona wakijadiliana na wengine kuhoji kwanini umeme unawekwa kwenye nyumba za tembe ambazo kuta zake zinatengenishwa na udongo.Kwangu naona wanaohiji hayo ni kama vile wamekosa hoja.

Watalaam wamejiridhisha na wanajua hakuna madhara yoyote kwani kuna vifaa maalum vinavyotumika katika kuunganisha umeme kwenye nyumba hizo.Nitoe rai kwa Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO endeleeni na majukumu yenu ya kuweka umeme vijijini.Kwa maisha ya sasa nishati ya umeme ambayo ni ya uhakika inahitajika sana kuliko nyakati nyingine zozote.Huo ndio ukweli.

Kwanini bibi na baba yangu waendelee kuteseka? Eti washindwe kuwa na luninga pale sebuluni kisa tu wapo kijijini.Eti waendelee tu kutumia vibatari .Hapana bwana lazima ifike mwisho.Walioko vijijini ni Watanzania na wana haki ya kupata umeme kama wengine wanaoishi maeneo ya mijini.

Tunafahamu kuna baadhi ya familia ambazo ziko mjini na zilishindwa kutembelea ndugu , jamaa na marafiki walioko vijijini na sababu tu ni kwamba eti wakienda huko hakuna umeme na wanasema hawawezi kutumia vibari.Kufungwa kwa umeme katika nyumba zetu za vijijini ambako wengi ndiko tunatokea, kunakwenda kufanya mabadiliko makubwa.

Mjini umeme upo na kijiji nako upo.Ukiishi kwenye ghorofa utakuwa na umeme na ukiishi kwenye nyumba ya tembe utakuwa na umeme.Hongereni TANESCO. Kufungwa umeme kwenye nyumba za vijijini kunakwenda kuifanya Tanzania kuwa yenye maendeleo.Kokote Mtanzania alipo na anahitaji umeme kwa ajili ya ujenzi wa maendeleo ya nchi yetu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameizindua nyumba ya Rose Kagoma iliyounganishiwa umeme wa REA katika Kijiji cha Ruganga Wilayani Kibondo.Katika hafla hiyo iliyofanyika Machi 24 mwaka huu, Waziri Kalemani amewataka Wandarasi kutokubagua Wananchi kwenye mradi huoKijiji cha Rugunga kimeunganishiwa umeme kupitia mradi wa umeme Vijijini wamu ya tatu sehemu ya kwanza(REA)



Hivyo makala KWA TANESCO HII MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU...

yaani makala yote KWA TANESCO HII MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU... Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KWA TANESCO HII MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU... mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/kwa-tanesco-hii-msema-kweli-mpenzi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KWA TANESCO HII MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU..."

Post a Comment

Loading...