Loading...

EMIRATES YATANGAZA OFA KWA WATANZANIA ZA KWENDA DUBAI

Loading...
EMIRATES YATANGAZA OFA KWA WATANZANIA ZA KWENDA DUBAI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa EMIRATES YATANGAZA OFA KWA WATANZANIA ZA KWENDA DUBAI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : EMIRATES YATANGAZA OFA KWA WATANZANIA ZA KWENDA DUBAI
link : EMIRATES YATANGAZA OFA KWA WATANZANIA ZA KWENDA DUBAI

soma pia


EMIRATES YATANGAZA OFA KWA WATANZANIA ZA KWENDA DUBAI


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la Ndege la Emirates limeamua kutoa ofa kwa Watanzania kutembelea Dubai ambapo ofa itapatikana katika daraja la biashara na uchumi ikiwa ni pamoja na mzigo wa tatu kuwa bure.

Taarifa ya Emirates iliyoitoa leo Machi 28,2019 kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam imesema kuwa ofa hiyo ni kwa tiketi ya daraja la uchumi kutoka Dar es Salam hadi Dubai inaanza $ 489 na daraja la biashara ya kuanzia $ 1,499 na kwamba ofa hizo zitatolewa kwa muda maalum na tiketi zinatakiwa kukatwa kuanzia Machi 26, 2019 na Aprili 9, 2019, safari zitaanza kati ya kati ya 26 Machi 26,  2019 na Septemba 30, 2019. Gharama ya tiketi ni pamoja na kodi ya uwanja wa ndege.

Pia Emirates inatoa ofa ya mzigo wa tatu bure mpaka kilo 23 kwa daraja la uchumi na kilo 32 kwa daraja la biashara huku ikifafanua watakaopata ofa hiyo watapata nafasi ya kuitembelea Dubai  ambapo kuna jua mwaka mzima, kuna maduka makubwa ya kutembelea, fukwe nzuri na majengo ya kipekee kwa familia nzima. 

"Wageni wa Dubai wanaweza kufurahia maeneo mengine ya jiji kwa kuona na kutembelea Hifadhi ya Kijiji cha Kimataifa - tamaduni mbalimbali na maeneo ya shopping - pamoja na viwanja vya mandhari kama Wild Wadi Waterpark na IMG World of Adventures,"imesema taarifa hiyo.

Emirates imesema kuwa katika Mji wa Dubai watatoa aina mbalimbali za malazi kukidhi bajeti zote na katika ndege zote za Emirates, wateja wanaweza kufurahia muda wa burudani kwenye mfumo wa burudani unaoweza kushinda tuzo inayoitwa ICE, ambayo inaonesha zaidi ya  vituo 4,000 vya burudani na ya kusikiliza na ya kuona, kutoka kwenye filamu za hivi karibuni na mziki.

Pia vitabu vya sauti na michezo, pamoja na bidhaa zinazopendwa na wanafamilia na huduma kwa watoto, ikiwepo ni pamoja na michezo ya kupendezwa, chakula cha watoto na sinema,familia zitapewa kipaumbele katika kutumia gari ya kumsukumia mtoto akifika uwanja wa Ndege wa Dubai.

Imesisitiza pamoja na huduma nzuri za kuingia na bidhaa, wateja wataweza kupokelewa vizuri na wafanyakazi wa kimataifa wa Emirates ambao hutokana na zaidi ya mataifa135 na ambao wanazugumza lugha zaidi ya 60, huku wakifurahia vyakula vya kikanda na kimataifa, kwa kutumia viungo vingi, ikifuatana na aina mbalimbali za mvinyo na vinywaji vingine.

"Tunawaomba Watanzania kuchangamkia ofa hii ambayo imekuja wakati muafaka , kikubwa ni kuhakikisha wananunua tiketi za Emirates kulingana na muda ambao umetolewa wa kipindi cha ofa.Kwa anayehitaji mawasiliano tafadhali anaweza kutembelea tovuti yetu ya www.emirates.com/tz au tembelea ofisi za Emirates au wakala wa usafiri,"imesema taarifa hiyo.



Hivyo makala EMIRATES YATANGAZA OFA KWA WATANZANIA ZA KWENDA DUBAI

yaani makala yote EMIRATES YATANGAZA OFA KWA WATANZANIA ZA KWENDA DUBAI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala EMIRATES YATANGAZA OFA KWA WATANZANIA ZA KWENDA DUBAI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/emirates-yatangaza-ofa-kwa-watanzania.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "EMIRATES YATANGAZA OFA KWA WATANZANIA ZA KWENDA DUBAI"

Post a Comment

Loading...