Loading...
title : FURSA ZAIDI ZATANGAZWA SEKTA YA KILIMO NA UWEKEZAJI
link : FURSA ZAIDI ZATANGAZWA SEKTA YA KILIMO NA UWEKEZAJI
FURSA ZAIDI ZATANGAZWA SEKTA YA KILIMO NA UWEKEZAJI
Na Mwandishi wetu, Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu ametangaza fursa za kiuchumi ndani ya Tarafa ya Mihambwe kwenye sekta ya kilimo na uwekezaji.
Gavana Shilatu aliyasema hayo kwenye kikao kilichohusisha Madiwani, Watendaji kata, Watendaji Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji, Wazee maarufu, Maafisa na wadau wa maendeleo kilichofanyika Leo Jumatatu Machi 4, 2019 katika ofisi ya Mtendaji kata Mihambwe ambapo amewakaribisha Wadau wa maendeleo kutumia vyema fursa za kiuchumi zilizopo ndani ya Tarafa ya Mihambwe.
Gavana Shilatu amezitaja fursa hizo kwenye sekta ya kilimo ardhi ya Mihambwe inafaa kwa kilimo cha Korosho, Mahindi, Mihogo, Alizeti, Mbaazi na Njugu.
Pia Gavana Shilatu amekaribisha wawekezaji wa viwanda vya kubangua Korosho waje wawekeze ndani ya Tarafa ya Mihambwe inayozalisha kwa wingi zao la Korosho.
Kama ambavyo Rais Dkt. John Pombe Magufuli anavyosisitiza Kauli mbiu ya "Hapa kazi Tu", Gavana Shilatu amewakaribisha Wadau wa maendeleo kuja kutumia vyema fursa zilizopo ndani ya Tarafa ya Mihambwe kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.
Hivyo makala FURSA ZAIDI ZATANGAZWA SEKTA YA KILIMO NA UWEKEZAJI
yaani makala yote FURSA ZAIDI ZATANGAZWA SEKTA YA KILIMO NA UWEKEZAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala FURSA ZAIDI ZATANGAZWA SEKTA YA KILIMO NA UWEKEZAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/fursa-zaidi-zatangazwa-sekta-ya-kilimo.html
0 Response to "FURSA ZAIDI ZATANGAZWA SEKTA YA KILIMO NA UWEKEZAJI"
Post a Comment