Loading...
title : WAHUJUMU WA ZAO LA KAHAWA MKOANI KAGERA WATAFUTE BIASHARA NYINGINE - RC GAGUTI
link : WAHUJUMU WA ZAO LA KAHAWA MKOANI KAGERA WATAFUTE BIASHARA NYINGINE - RC GAGUTI
WAHUJUMU WA ZAO LA KAHAWA MKOANI KAGERA WATAFUTE BIASHARA NYINGINE - RC GAGUTI
Anaandika Abdullatif Yunus - Karagwe
Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti imesema haitafumbia macho wale wote wenye mpango wa kuhujumu zao la Kahawa Mkoani Kagera kwa kununua na kuuza kahawa ya magendo, kahawa changa (butula), na wale wote wenye nia ya kuhujumu Biashara hiyo kwa namna yoyote ile katika msimu unaokwenda kuanza Mapema mwezi Mei mwaka huu.
Akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 32 wa Chama Kikuu cha Ushirika Wilayani Karagwe na Kyerwa Karagwe Development Cooperative Union Limited (KDCU LTD) Mkuu wa Mkoa Gaguti katika Ukumbi wa CCM Kayanga Machi 05, 2019, amesema kwa msimu uliopita kuna baadhi ya Viongozi wamehusika katika kuhujumu zao la Kahawa kwa kunufaisha matumbo yao na sasa hatua za haraka zitachukuliwa ili kuhakikisha Mkulima ananufaika na Kahawa yake.
Mh. Gaguti amesema Serikali inatambua changamoto ya Bei ya Zao la Kahawa ni ya wadau wengi, lakini kama Serikali itatimiza wajibu wake wa kuendelea kukutana na kuwashirikisha wadau wote wa kahawa kujadili suala hili, huku na KDCU nao kama chama Kikuu kuweka taratibu zao za uberoshaji wa Zao hilo kuanzia katika Vyama vya msingi, na adhma yake ni kuona zao hilo linauzwa katika mifumo rasmi iliyoratibiwa na chama Kikuu, huku takwimu zikionyesha kwa msimu uliopita Mkoa ulikusanya Kahawa kilo Milioni 58. 9 ambapo KDCU Ltd walikusanya Kilo milioni 39 sawa na 67%.
Awali kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Karagwe Mh. Godfrey Mheluka Amewakumbusha wajumbe wa mkutano Mkuu juu ya mfuko wa Bima ya Afya na Mazao yote ya Ushirika uliozinduliwa Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na hivyo kuwataka wanachama wote wa KDCU kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na yale yote yatokanayo na mfuko huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 32 wa KDCU LTD (hawapo pichani) Mjini Kayanga Wilayani Karagwe.
Mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka akisisitiza jambo wakati akitoa salaamu zake kabla ya Kumkaribisha Mgeni rasmi katika Mkutano wa 32 wa KDCU LTD.
Pichani ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Kagera Ndg Hamim Mahamudu akisisitiza juu ya kuimarisha Ushirika, ili kupitia Ushirika huo Mkulima aweze kupambana na Maadui watatu ambao ni Ujinga, Maradhi na Umasikini.
Pichani ni sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KDCU LTD wakiendelea kufuatilia Mkutano huo katika Ukumbi wa CCM Kayanga Karagwe
Hivyo makala WAHUJUMU WA ZAO LA KAHAWA MKOANI KAGERA WATAFUTE BIASHARA NYINGINE - RC GAGUTI
yaani makala yote WAHUJUMU WA ZAO LA KAHAWA MKOANI KAGERA WATAFUTE BIASHARA NYINGINE - RC GAGUTI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAHUJUMU WA ZAO LA KAHAWA MKOANI KAGERA WATAFUTE BIASHARA NYINGINE - RC GAGUTI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/wahujumu-wa-zao-la-kahawa-mkoani-kagera.html
0 Response to "WAHUJUMU WA ZAO LA KAHAWA MKOANI KAGERA WATAFUTE BIASHARA NYINGINE - RC GAGUTI"
Post a Comment