Loading...
title : HALI YA UJANGILI YAPUNGUA NCHINI, JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZAPONGEZA
link : HALI YA UJANGILI YAPUNGUA NCHINI, JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZAPONGEZA
HALI YA UJANGILI YAPUNGUA NCHINI, JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZAPONGEZA
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA) imesema kiwango cha Ujangili kimeshuka hadi kupelekea kupata maoni mbalimbali ya Wadau kutoka Jumuiya za Kimataifa, kutokana nakufanyika kazi kubwa ya kuzuia ujangili huo.
Takwimu zinaonyesha kuwa Ujangili umeshuka ukilinganisha na miaka ya nyuma. Ujangili wa Wanyamapori unafanywa kwa Wanyama wanaowindwa zaidi, Mfano Tembo, katika Hifadhi ya Selous inayoongoza kuwa na Tembo wengi zaidi inaonyesha mwaka 2014/2015 waliuawa Tembo 18, 2015/2016 Tembo 16, 2016/2017 Tembo 7 na 2017/2018 hakuna idadi yoyote ya Tembo aliyeuawa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Siku ya Wanyamapori Duniani, Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Dkt. James Wakibara amesema Serikali imeweka nguvu kubwa kupiga vita Ujangili nchini ikiwa sambamba nakuanzishwa kwa 'Wildlife Crime Task Force' itakayokuwa inatafuta Wahalifu wanaojiusisha na Ujangili sehemu yoyote hapa nchini.
"Kwa sasa suala la Ujangili tunapumua, sio kama miaka ya nyuma, Ujangili wa Watu kukimbiza Wanyama kwa ajili ya kula, huu hauathiri sana tafauti na Ujangili wa kuuwa Wanyama kwa ajili ya Biashara ndio changamoto hapa nchini", amesema Dkt. Wakibara.
Dkt. Wakibara amesema Wanyamapori wachululiwe kama rafiki wa mazingira, rafiki wa Uchumi kwa nchi, rafiki wa Uchumi wa maisha yao.
Amesema mwaka 1982, Hifadhi ya Selous iliingizwa kwenye Urithi wa Dunia kwa kuwa Tembo 106, 000, idadi hiyo imefanya kuingizwa kwenye Urithi huo, wakati Miaka minne iliyopita Tembo hao walishuka hadi 13, 500 sawa na 87%.
Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Utalii na Huduma za Biashara - TAWA, Imani Nkuwi amesema maeneo madogo yanayofahamika kama Vitaru vya Uwindaji, kwa sasa yameanza kugaiwa kwa utaratibu mpya kwa Mfumo wa Kieletroniki kwa njia ya mnada, amesema wakati wowote Vitaru 81 vitaanza kugaiwa baada ya Kamati kuidhinisha Utaratibu huo, kunadi Vitaru hivyo kwa utaribu wa Kieletroniki.
Nkuwi amesema Mapato ya Serikali yalishuka kutokana na Vitaru hivyo kuwa wazi, mapato yalishuka kwa 10% kwa sababu yakurudishwa kwa Vitaru hivyo.
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Dkt. James Wakibara akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Dunia yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala HALI YA UJANGILI YAPUNGUA NCHINI, JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZAPONGEZA
yaani makala yote HALI YA UJANGILI YAPUNGUA NCHINI, JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZAPONGEZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HALI YA UJANGILI YAPUNGUA NCHINI, JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZAPONGEZA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/hali-ya-ujangili-yapungua-nchini.html
0 Response to "HALI YA UJANGILI YAPUNGUA NCHINI, JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZAPONGEZA"
Post a Comment