Loading...
title : HESLB yaweka mikakati ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita.
link : HESLB yaweka mikakati ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita.
HESLB yaweka mikakati ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) iko katika mkakati wa utoaji wa elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita ili kuweza wanafunzi hao waelewe namna ya kujaza fomu kwa usahihi wakati wa kuomba mikopo katoka bodi hiyo.
Wakizungumza na wanafunzi katika shule za Sekondari za St.Anthony, Kisutu na Zanaki wamesema kuwa wakati wa kuomba mikopo wanafunzi wamekuwa wanafanya makosa ambapo Bodi imeona kuna umhimu wa kuwapa elimu wanafunzi.
Afisa wa Bodi hiyo Daud Elisha amesema elimu wanayoitoa kwa wanafunzi ni kutokana na kuwepo kwa makosa baadhi ya wanafunzi wakati wa uombaji wa mikopo.
Elisha amesema lengo la bodi kuona wanafunzi wa kidato cha sita wanapata uelewa mapema namna ya kuomba mikopo ya bodi kwa vigezo vilivyowekwa.
Aidha amesema elimu wanayoitoa ni mwendelezo kwa nchi nzima katika kuhakikisha kila mwanafunzi anajua kinagaubaga kuhusiana na bodi inavyofanya kazi katika utoaji mikopo kwa wanafunzi wahitaji wa kitanzania.
"Tumedhamiria kutoa elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita pindi wanapohitimu na kujiunga na elimu ya juu wakiomba mkopo wa wasiwe na changamoto ya kufanya ashindwe kuomba mkopo huo"amesema Elisha.
Nae Afisa Mikopo wa Bodi Christina Chacha amesema kuwa licha ya kuwapa elimu ya wanafunzi kuhusiana na uombaji mkopo pia wanatoa elimu ya namna ya kurejesha mkopo huo kwa wale watakaonufaika.
Amesema mkopo wanayotoa kwa wanafunzi kwa ajili ya elimu ya juu lazima ilipwe kwa ajili wengine kukopeshwa.
Aidha maswali ya wanafunzi wengi yalijikita endapo mwanafunzi atapohitimu shahada yake na akawa hajaajiriwa ataulipaje mkopo ambapo bodi hiyo imesema kukosa kazi sio kigezo cha kutolipa mkopo kwani elimu hiyo anaweza kufanya kazi nyingine na kuweza kulipa mkopo huo.
Afisa wa HESLB Daud Elisha akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari kisutu kuhusiana na vigezo vya uombaji mikopo katika bodi hiyo.
Wanafunzi wa kidato cha sita Shule ya Sekondari Zanaki wakisikiliza maelezo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) .
Afisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Daud Elisha akizungumza na wanafunzi wa kidato cha Sita Shule ya Sekondari Kisutu wakati Bodi hiyo ilipokwenda kutoa elimu ya masuala mbalimbali ya namna wanafunzi wanavyoweza kuomba mkopo katika Bodi hiyo.
Afisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Christina Chacha akitoa maelezo kwa wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Kisutu kuhusu vigezo vya uombaji mikopo na masharti ya mkopo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Zanaki Julieth Matowo akitoa maelezo wakati Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ilipokwenda kutoa elimu katika shule hiyo.
Wanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Kisutu wakisikiliza mada kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
Hivyo makala HESLB yaweka mikakati ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita.
yaani makala yote HESLB yaweka mikakati ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HESLB yaweka mikakati ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/heslb-yaweka-mikakati-ya-utoaji-elimu.html
0 Response to "HESLB yaweka mikakati ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita."
Post a Comment