Loading...

HESLB:Sio wote wanahitaji mkopo wa elimu ya juu

Loading...
HESLB:Sio wote wanahitaji mkopo wa elimu ya juu - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HESLB:Sio wote wanahitaji mkopo wa elimu ya juu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HESLB:Sio wote wanahitaji mkopo wa elimu ya juu
link : HESLB:Sio wote wanahitaji mkopo wa elimu ya juu

soma pia


HESLB:Sio wote wanahitaji mkopo wa elimu ya juu

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema utoaji wa mikopo unazingatia vigezo kwa wenye uhitaji wa mkopo huo kwa ajili ya kusoma elimu ya Juu na wengine sio wahitaji wa mkopo kutokana na hali za familia zao.
 
Hayo yamesemwa na Afisa wa Bodi hiyo Christina Chacha wakati Bodi hiyo ilipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika Shule ya Sekondari Jitegemee, amesema kuwa mikopo haitolewi kwa wanafunzi kwa sababu ameomba kinachoangaliwa ni uhitaji msingi ambapo mwanafunzi huyo asipopata mkopo hawezi kuendelea na elimu ya juu.

Amesema kuwa kuna baadhi ya wazazi wanabudu gharama za kusomesha watoto hivyo wengine ambao kwa sababu mbalimbali hawezi kumudu ikiwemo umasikini na wakati mwingine ulemavu hivyo serikali inachukua jukumu ya kumkopesha mwanafunzi anayotoka familia hiyo.

Chacha amesema kuwa kuna wanafunzi wengine ni walemavu na familia zao ni masikini kwa vigezo hivyo anakuwa sehemu ya mhitaji mkopo kutoka bodi.
Aidha Chacha amesema kuwa mkopo wa bodi kwa wanafunzi wa elimu ya juu wote ila sifa yake ni kuwa Mtanzania bila kujali shule ya serikali au binafsi na kuzingatia ufaulu wowote.

Amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sanaa wanahisi kama wanabaguliwa wakati bodi inawaangalia wote kwa jicho moja kwa kwani wote wakihitimu shahada zao wanaijenga nchi."Tunatoa elimu hii ya uombaji mikopo ili muweze kujaza fomu zetu kwa usahihi na kurahisha bodi kutumia muda mdogo katika kupanga mikopo na shughuli zingine zikaendelea"amesema Chacha.

Mwanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Jitegemee Abdul Shafii amesema kuwa ujio wa bodi umetoa hofu katika uombaji mikopo kutokana na kupata taarifa zisizo sahihi.

Amesema elimu walioipata kutoka bodi ni muda mwafaka hivyo atatumia maelekezo hayo wakati wa kuomba mkopo.
 Afisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Christina Chacha akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa elimu ya uombaji wa mkopo wa elimu ya juu kwa wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Jitegemee.
 Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Shule ya Sekondari Jitegemee wakisilikiza bodi ya Mkopo ya Wanafunzi wa Elimu Juu (HESLB)
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Jitegemee Abdul Shafii akitoa maelezo namna walivyopokea elimu ya uombaji mkopo katika Bodi ya Mkopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)


Hivyo makala HESLB:Sio wote wanahitaji mkopo wa elimu ya juu

yaani makala yote HESLB:Sio wote wanahitaji mkopo wa elimu ya juu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HESLB:Sio wote wanahitaji mkopo wa elimu ya juu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/heslbsio-wote-wanahitaji-mkopo-wa-elimu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "HESLB:Sio wote wanahitaji mkopo wa elimu ya juu"

Post a Comment

Loading...