Loading...
title : Ukatili wa Kijinsia wilayani Kisarawe bado changamoto.
link : Ukatili wa Kijinsia wilayani Kisarawe bado changamoto.
Ukatili wa Kijinsia wilayani Kisarawe bado changamoto.
Ukatili wa Kijinsia kwa Wilaya ya Kisarawe bado changamoto katika upande Mimba za Utotoni.
Wanaume ambao wanawasababishia mimba watoto wanakimbia kwa kisingizio cha kukosa kipato cha kulea familia.
Mbali na ukatili huo pia kumekuwa na kasi kubwa ya kesi za Ubakaji na ulawiti zinazoripotiwa mara kwa mara katika dawati la Jinsia la wilaya ya Kisarawe na Ofisi ya Ustawi wa Jamii ya wilaya hiyo.
Akizungumza katika Semina ya muendelezo wa Maadhimisho ya Siku ya Wnawake Duniani wilayani Kisarawe mkoani Pwani iliyoandaliwa na Taasisi ya Bright Jamii Initiative Ofisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya hiyo Mwandili Rangi amesema ukatili huo umekuwa ukiripotiwa katika ofisi yake na kusaidia kutatua baadhi ya migogoro na mengine kuipeleka katika mahakama ya mwanzo.
"Kisarawe bado ukatili wa kijinsia upo Kwa kiasi kikubwa wanawake wanapigwa,Masuala ya Ubakaji,Unyanyasaji,Mama na Mtoto kutelekezwa hali inayofanywa mtoto kukosa haki zake za msingi," amesema Rangi
Rangi amesema wanawake wamekuwa wakipigwa sana na kutelekezwa na watoto haki inayofanya wanamke kuangaika na mtoto alieachiwa."Wanaume wa Kisarawe wanakwepa majukumu sana ya kuhudumia familia zao,utakuta anampa mtu ujauzito...mwanamke akijifungua anamkimbia mtoto na Mama mtu,"amesema
Naye Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi ya Bright Jamii Initiative,Godwin Mongi alisema Mila na desturi zimekuwa zikimbadilisha mwanamke fikra na kuona ukatili wa kijinsia ni hali ya kawaida.
Amesema hali hiyo imefikia baada ya kuona Jamii kubwa inaona Mwanaume ndio mwenye hali kuliko mwanaume tangu mwanamke anapozaliwa na kukuta mfumo huo.
" Wadau mbalimbali tukishirikiana Kwa pamoja tutahakikisha tunadhibiti hali hio ya ukatili wajinsia...sisi tumeona tube Kisarawe kuanza programu hii kutokana na hali ya ukatili wa kijinsia bado kuwepo na hii ni muendelezo wa kusherekea Siku ya mwanamke duniani,"alisema Mongo
Naye Afisa Polisi wa Dawati la Jinsia Sagenti Frida Mbise amesema dawati lao limekuwa likipokea kesi za mimba za utotoni zinazohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 14 hadi17.
Semina hiyo ilishirikisha Viongozi wa Dini,viongozi wa erikali,Wajasiliamari pamoja na Jeshi la Polisi.
Picha ya pamoja ya viongozi mbalimbali wakiwa katika mwendelezo wa maadhimisho y siku ya wanawake duniani wilayani Kisarawe.
Hivyo makala Ukatili wa Kijinsia wilayani Kisarawe bado changamoto.
yaani makala yote Ukatili wa Kijinsia wilayani Kisarawe bado changamoto. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Ukatili wa Kijinsia wilayani Kisarawe bado changamoto. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/ukatili-wa-kijinsia-wilayani-kisarawe.html
0 Response to "Ukatili wa Kijinsia wilayani Kisarawe bado changamoto."
Post a Comment