Loading...
title : HUWEZI KUBADILI HATI MILIKI KAMA UMEANDIKIA MKATABA SERIKALI ZA MITAA.
link : HUWEZI KUBADILI HATI MILIKI KAMA UMEANDIKIA MKATABA SERIKALI ZA MITAA.
HUWEZI KUBADILI HATI MILIKI KAMA UMEANDIKIA MKATABA SERIKALI ZA MITAA.
Hapo awali niliandika namna sheria isivyowaruhusu viongozi wa serikali za mitaa (watendaji kata, wenyeviti wa mitaa,wajumbe, na ule uongozi wote wa huko chini) kuandaa na kusimamia mauzo na manunuzi ya nyumba au viwanja, kwa ujumla ardhi. Nikasema kuwa kitu hicho hakiruhusiwi katika sheria na wanaofanya hivyo wako katika makosa makubwa.
Nikasema zaidi kuwa, na asilimia kumi wanayowatoza ni makosa na ndio maana hailipwi kwenye akaunti ya serikali bali mkononi au utapewa risiti za kuchana kwenye daftari badala ya EFD, wizi mtupu.
Leo tena tutizame kama unaweza kuruhusiwa kubadili jina la ardhi kutoka kwa aliyekuuzia kwenda kwenye jina lako mnunuzi ikiwa ulisimamiwa na serikali za mitaa katika manunuzi hasa ardhi iliyopimwa.
Sheria Namba 4 ya 1999, Sheria ya Ardhi kifungu cha 62( 1) kinasema kuwa kila nyaraka(document) yoyote ya ardhi iliyosajliwa ambayo itatumika katika mauzo,rehani,zawadi,kurithi, au pango ni lazima iwe katika mfumo wa fomu maalum. Kifungu hiki kinaturejesha katika kanuni za ardhi za mwaka 2001 ili kuziona fomu zinazohusika katika manunuzi ya ardhi na mahitaji yake.
Fomu ya kwanza ni fomu namba 38 ambayo ni sawa na mkataba wa mauzo(contract for disposition). Fomu hii inalazimisha kuwa ni lazima iwe imegongwa muhuri wa Wakili au kushudiwa na wakili.
Fomu ya pili ni namba 35 ambayo kisheria ni nyaraka ya kuhamisha umiliki(transfer of right of occupancy).Fomu hii nayo inatoa ulazima wa kuwa imeshuhudiwa na kugongwa muhuri wa Wakili pande mbili, yaani upande wa mhamisha umiliki/muuzaji, na upande wa mpokea umiliki/mnunuzi.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
Hivyo makala HUWEZI KUBADILI HATI MILIKI KAMA UMEANDIKIA MKATABA SERIKALI ZA MITAA.
yaani makala yote HUWEZI KUBADILI HATI MILIKI KAMA UMEANDIKIA MKATABA SERIKALI ZA MITAA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HUWEZI KUBADILI HATI MILIKI KAMA UMEANDIKIA MKATABA SERIKALI ZA MITAA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/huwezi-kubadili-hati-miliki-kama.html
0 Response to "HUWEZI KUBADILI HATI MILIKI KAMA UMEANDIKIA MKATABA SERIKALI ZA MITAA."
Post a Comment