Loading...

IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU

Loading...
IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU
link : IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU

soma pia


IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), walipomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta alipomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne A. Sagini (wa pili kushoto) akifurahia jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kushoto) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati), baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Simiyu (watatu wa mwanzo kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tano kulia) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta(kulia) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi , kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto), akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kushoto) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Mwenyekiti wa RAAWU Taifa, Dkt. Micahel Mawondo akizungumza jambo wakati Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kushoto) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi , kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne A. Sagini (katikati), baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Simiyu (watatu wa mwanzo kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kulia mbele) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinatarajia kujenga Tawi jipya katika Kata ya Sapiwi Tarafa ya Dutwa wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

Viongozi wa chuo hicho wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Tadeo Andrew Satta wametembelea eneo hilo Machi 26, 2019 na baadaye kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa Mkoa wa Simiyu ambapo wamekubaliana kushirikiana katika hatua zote kuanzia upimaji wa eneo mpaka ujenzi wa majengo ya chuo.

Akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Andrew Satta amewashukuru viongozi hao kwa kutoa eneo la ekari ishirini bure akaahidi kushirikiana na Serikali mkoani hapa kuhakikisha tawi hilo linajengwa mkoani Simiyu ili kusogeza karibu huduma kwa wananchi wa Simiyu.

Awali akizungumza na viongozi hao Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo iko tayari kushirikiana na viongozi wa Chuo hicho kwa kutoa wataalam watakaosaidia katika Usimamizi wa upimaji na akashauri ujenzi wa majengo ya chuo hicho ufanyike kwa kutumia mfumo wa ‘Force Account’ ili kupunguza gharama.

Amesema mfumo huu utapunguza gharama kwa kuwa hautumii wakandarasi badala yake ujenzi utafanywa na mafundi wa kawaida wakisimamiwa na wahandisi wa ujenzi Mkoa na Halmashauri mkoani Simiyu huku vifaa vyote vya ujenzi vikinunuliwa kwa pamoja na chuo hicho.

Aidha, amemhakikishia upatikanaji wa wanafunzi kwa kuwa hadi sasa Mkoa wa Simiyu bado una Vyuo vichache vya elimu ya juu, huku akibainisha kuwa tayari Serikali mkoani hapa imeshatoa ardhi bure kwa ajili ujenzi wa Matawi ya Vyuo mbalimbali vya elimu ya juu ikiwemo Chuo cha Mipango, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo cha Mahakama.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema wanaendelea kushawishi Taasisi nyingi za Elimu ya Juu kujenga matawi yake Mkoani hapa, ili kutoa nafasi kwa Wanasimiyu kupata elimu ya juu itakayochangia kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii


Hivyo makala IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU

yaani makala yote IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/ifm-kujenga-tawi-jipya-simiyu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU"

Post a Comment

Loading...