Loading...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA

Loading...
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA
link : KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA

soma pia


KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA

 Jengo la Mahakama ya wilaya ya Rungwe na Mahakama ya Mwanzo ya Rungwe mjini likiwa katika hatua za awali za ujenzi. jengo hili linajengwa na Mkandarasi M/S Moladi Tanzania Ltd na kusimamiwa na Chuo Kikuu cha Ardhi kama Mtaalam Mshauri. Ujenzi ulianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2017/2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili 2019. Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walitembelea na kukagua ujenzi wa jengo hili leo mkoani Mbeya.
 Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania Bwn Khamadu Kitunzi akiwaelezea waheshimiwa wabunge kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo ya Mahakama.
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisikiliza ufafanuzi juu ya mradi wa ujenzi wa Mahakama kutoka kwa Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania Bwn Khamadu Kitunzi (hayupo pichani) walipoongozana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi huo.


 Jengo la Mahakama ya Mwanzo Uyole likiwa katika hatua za ukamilishwaji (finishing) Jengo hili linajengwa na Mkandarasi M/S PIM Innovators na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Mbeya. Ujenzi ulianza Desemba mwaka jana na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili 2019. Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walitembelea na kukagua ujenzi wa jengo hili leo mkoani Mbeya.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Uyole.Lydia Churi Ntambi.




Na Lydia Churi- Mahakama-Mbeya


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wameanza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Tanzania inayoendelea nchini ambapo leo wajumbe hao wametembelea miradi iliyopo wilayani Rungwe pamoja na Uyole jijini Mbeya. 

Pamoja na wajumbe wa kamati hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome pia walikuwa ni miongoni mwa watu walioshiriki kwenye ziara hiyo. 

Katika ziara hiyo mkoani Mbeya, wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria walianza kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa Mahakama ya wilaya ya Rungwe ambao bado uko katika hatua za awali. 

Mradi huu uliopangwa kutekelezwa mwaka 2017/2018 unahusisha huduma za mahakama ya wilaya na ya Mwanzo mjini Rungwe ambao unatekelezwa na Mkandarasi M/S Moladi Tanzania Ltd na kusimamiwa na Chuo kikuu cha Ardhi kama Mtaalamu Mshauri. 

Aidha, Mradi wa Ujenzi wa Mahakama ya wilaya na ya Mahakama ya Mwanzo Rungwe mjini ulianza kutekelezwa mwaka jana na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili mwaka huu. 

Baada ya kutembelea ujenzi wa Majengo ya Mahakama wilayani Rungwe, wajumbe wa Kamati hiyo pia walitembelea ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Uyole ulioanza kutekelezwa Desemba 2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi April mwaka huu. 

Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi M/S PIM Innovators na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Mbeya kama Mtaalamu Mshauri. Hatua iliyofikiwa sasa ni kuezeka na kuanza kazi za umaliziaji( finishing) 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pia wanatarajia kutembelea na kukagua ujenzi wa Mahakama katika mkoa wa Arusha na Manyara.


Hivyo makala KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA

yaani makala yote KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/kamati-ya-kudumu-ya-bunge-ya-katiba-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA"

Post a Comment

Loading...